Mambo ambayo hupaswi kuwaambiwa polisi wa Kenya baada ya kukamatwa

Muhtasari
  • Mambo ambayo hupaswi kuwaambiwa polisi wa Kenya baada ya kukamatwa
Image: Maktaba

Wadau najua wikendi imefika, na wengi wanapanga kuenda kujivinjari kwa njia tofauti, lakini cha muhimu ni kuwa chunga usjipate katika upande mbaya na polisi.

Je umewahi japata upande mbaya na polisi na ukahisi hujatendewa haki?

Najua baadhi ya watu wengi wana cha kusema, baada ya kujipata upande mbaya na polisi na kisha wanajifanya kuwa wao ni werevu, na ujifanya hawajakosa.

Katika makala haya tunazingatia mambo ambayo hupaswi kuambia polisi baada ya kukamatwa.

Baada ya kukamatwa usijifanye mjanja au mjuaji sana kuliko polisi, lakini nyenyekea na utulie hadi pale utaambiwa unaweza kuzungumza.

Mamb hayo ni kama;

1.Najua haki yangu

Ni usemi ambao unatumiwa sana na wananchi baada ya kukamatwa huku usemi huo ukiwafanya maafisa wengi kupandwa na hasira.lakini swali ni je kama unajua haki yako kwa niini ukapatwa katika upande mbaya?

Kama unataka maisha yako yawe sambamba baada ya kukamatwa usitoe neno la unajua haki yako kwenye kinwa chako.

2.Unajua baba yangu ni nani?

Ni usemi ambao unasemwa sana na vijana wakikamatwa, haijalishi baba yako ni nani kama umepatikana na makosa au upande mbaya na polisi lazima haki ifanyike, kwa maana hamna mtu ambaye yuko juu ya sheria.

3.Onyesha kitambulisho chako cha kazi

Ala! ndio matapeli wamekuwa wengi ata wengine wanavalia nguo za polisi ilhali wao hawana ujuzi wowote kuhusu polisi, lakini kama umepatikana na makosa kwa nini uulize kitambulisho?

4.Usinishike hivyo!

Wakati mwingine polisi watakunyanyua juu kwa juu, lakini ukijaribu kumfundisha jinsi ya kukushika haya basi utanyanyuliwa vivlivyo.

5.Umesoma katiba wewe?

Kwa kweli kosa lako na katiba zinaingiliana wapi, ndio wengi wamesoma lakini kwa nini uulize swali kama hilo?Wengi wao wanaweza kuwa hawajasoma lakini usijaribu kuwaeliemisha kuhusu katiba ya mwaka wa 2010.

6.Unanijua mimi ni nani?

Usemi ambao polisi wengi wanachukia kuusikia kwani kama wewe ni mzuri kwa nini upatikane katika upande mbaya na sheria?

Haya basi swli ni je umewahi sema mambo hayo, na kama uliyasema mbele ya polisi nini haswa kilikutendekea?

Basi wikendi hii kama utajipata upande mbaya na polisi jaribu kujitete vingine na wala sio kuwaudhi polisi. Lakini cha muhimu ni mjichunge kwani maisha ni muhimu sana.