Zifahamu nchi 6 ambazo idadi ya wafungwa huongezeka maradufu kuliko uwezo wa magereza

Muhtasari

•Kuna mataifa sita ambapo idadi ya wafungwa ni mara mbili, mara tatu au mara nne zaidi ya nafasi iliyopo ya uwezo wa kuwahifadhi. Nchi hizi kijiografia ziko katika eneo lote la ukanda: mbili za Amerika Kusini, mbili za Amerika ya Kati, na mbili za Caribbean.

Image: GETTY IMAGES

Mauaji ya hivi karibuni yaliyotokea gerezani huko Ecuador - mabaya zaidi katika historia ya nchi hiyo, ambayo yalisababisha watu wasiopungua 119 kufa - imeangaziwa tena shida ya msongamano wa wafungwa.

Wataalamu wengi wameelezea kwamba kiwango cha kukaa wafungwa gerezani huko Ecuador,kwa 133%, kilikuwa moja ya sababu zilizosababisha msiba huo mkubwa.

Magereza 52 ya Ecuador yanahifadhi zaidi ya wafungwa 39,000, karibu 10,000 zaidi ya wanaoweza kukidhi, kwa mujibu takwimu rasmi kuhusu uwezo wa magereza.

Ghasia huko Guayaquil zilikuwa za tatu kurekodiwa katika gereza la Ecuador mwaka 2021, baada ya zile zilizotokea mnamo Februari na Julai, ambazo zilisababisha vifo79 na 22, mtawalia.

Hatahivyo, nchi hiyo ya Amerika Kusini ndio yenye magereza mengi katika eneo hilo.

Ecuador haiko hata katika "10 bora" ya nchi za Amerika Kusini na Carribean zilizo na magereza yaliyojaa zaidi.

Katika orodha ya World Prison Brief (WPB), hifadhidata inayoongoza ulimwenguni juu ya masuala ya magereza, ambayo imekusanywa na Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Uhalifu na Sheria (ICPR) nchini Uingereza, Ecuador Imeorodheshwa nambari 18 katika ukanda huo.

Ili kupata picha kamili ya ukubwa wa tatizo hilo, inatosha kuona kwamba ni nchi moja tu huko Amerika Kusini ambayo haina gereza kamili: Suriname, taifa lenye watu wachache zaidi katika bara, ambapo kiwango cha wafungwa gerezani kinafikia 75.2%.

Chile inafuata ya pili kutoka chini, na kiwango cha 100.4%. Kitu kama hicho hufanyika Amerika ya Kati: huko Belize tu huepuka kujazana kwa idadi ya watu, ikiwa na kiwango cha 49.8% tu, na Mexico inafuata na 101.8%.

Image: GETTY IMAGES

Lakini kinachoshangaza zaidi kuhusu takwimu sio tu uwepo wa idadi ICPR inakadiria kuwa udhibiti wa wastani wa ukanda ni 160%. Lakini, kwa kuongezea, katika nchi nyingine idadi ya wafungwa ni mara mbili, tatu na hata mara nne kuliko uwezo.

Nchi sita zenye idadi kubwa ya wafungwa kuliko uwezo

Kuna mataifa sita ambapo idadi ya wafungwa ni mara mbili, mara tatu au mara nne zaidi ya nafasi iliyopo ya uwezo wa kuwahifadhi. Nchi hizi kijiografia ziko katika eneo lote la ukanda: mbili za Amerika Kusini, mbili za Amerika ya Kati, na mbili za Caribbean.

Ile iliyo na hali mbaya zaidi, ni Haiti, nchi masikini kabisa katika bara la Amerika, ambayo wafungwa waliojaaa kwa 454.4%.

Inafuatwa na Guatemala, ambayo inazidisha uwezo wa mfumo wake wa magereza, ikiwa na watu kwa 367.2%, na Bolivia,kwa 269.9%.

Mataifa haya matatu ni kati ya kumi yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani.

Image: GETTY IMAGES

Grenada (233.8%), Peru (223.6%) na Honduras (204.5%) zinakamilisha jedwali la nchi za Amerika Kusini na carribean na idadi ya wafungwa ambao huongezeka mara mbili kuliko uwezo.

Kwa nini nchi hizi, na Amerika Kusini kwa ujumla, zina shida kubwa ya msongamano wa wafungwa? Wataalam ambao BBC Mundo walizungumza nao wanathibitisha kwamba, ingawa kila taifa lina shida zake, kuna mambo kadhaa ambayo yanasababisha.

Si upungufu wa magereza

Hakika jambo la kwanza ulilofikiria ni kwamba shida kuu ni kwamba hakuna magereza ya kutosha yaliyojengwa.

Na ni kweli, kwa sehemu tu. Ukuaji wa idadi ya wafungwa imekuwa kubwa zaidi, na haraka sana, kuliko kuongezeka kwa miundombinu inayofanya kazi kuidhibiti.

Lakini wasomi wa suala hilo wanasema kuwa kujenga magereza zaidi hakutatatua shida ya msongamano.

"Tunajua kwamba magereza zaidi ambayo yamejengwa, ndivyo yatakavyojazwa zaidi.

Majaji huwa kwenye shinikizo katika suala hilo," anasema Sacha Darke, profesa wa masuala ya uhalifu katika Chuo Kikuu cha Westminster, Uingereza, ambaye ni mtaalamu wa mifumo ya magereza nchini Uingereza na Amerika Kusini. Darke anaamini kuwa shida sio idadi ya magereza, bali idadi ya wafungwa.

Anaangazia kuwa idadi ya wafungwa katika eneo hilo imeongezeka mara tatu tangu 2000, na anaiita Amerika Kusini "eneo jipya la kufungwa kwa watu wengi." "Itapita Amerika Kaskazini," anasema, akimaanisha eneo lenye wafungwa wengi ulimwenguni.

''Hivi leo Merekani ina idadi kubwa ya wafungwa duniani, idadi ya watu (zaidi ya milioni 2), na kwa kiwango cha wafungwa kwa idadi ya idadi ya watu ni(wafungwa 629 kwa kila wakazi 100,000).

Kuna watu wengi katika magereza ya Marekani kuliko katika nchi zote za Amerika Kusini na Carribean pamoja. Lakini msomi huyo anasisitiza kwamba, wakati Marekani ilifikia rekodi hiyo ya wafungwa milioni 2 zaidi ya miongo miwili iliyopita - na tangu wakati huo idadi hiyo haijakua - wakati huo huo katika Amerika ya Kusini idadi ya wafungwa ilitoka 650,000 hadi milioni 1.7.

Changamoto ya mfumo wa mahakama

"Shida kuu ni kwa mfumo wa kupatikana haki, na si mfumo wa magereza, ambao hauamui ni nani aliyepo," César Muñoz, mtafiti mwandamizi katika idara ya Amerika ya Kusini ya Haki za Binadamu (HRW), anaiambia BBC Mundo. Muñoz anaelezea mapungufu mawili ya haki: ucheleweshaji na "matumizi ya kiasi kikubwa ya vizuizi."

Image: GETTY IMAGES

Kwa wastani, zaidi ya 40% ya wafungwa Amerika Kusini wanashikiliwa bila kushtakiwa. Amerika ya kati wastani ni 35%.

Ikiwa tunaongezea kwenye ukweli kwamba michakato ya kimahakama katika nchi nyingi huchukua miaka, mtu huanza kuelewa ni kwanini magereza hujaza wafungwa kuliko uwezo wake.

Sera ya kupambana na madawa ya kulevya

Jambo la hivi karibuni ambalo ni muhimu kuelewa ni kwanini wafungwa wa Amerika Kusini wameongezeka kwa miaka michache, wataalamu wanasema.

"Leo moja ya sababu kuu za kuwa jela ni uuzaji wa dawa za kulevya," anasema Darke. "Lakini watu wengi waliokamatwa sio wafanyabiashara wa dawa za kulevya, lakini vijana ambao huwa madalali wanaounganisha kati ya wale wanaouza na kununua," anasema, akimaanisha kile kinachojulikana kama "kuuza madawa ya kulevya."

"Katika Amerika Kusini, kila mtu anayeuza dawa za kulevya huitwa mfanya biashara, lakini huko Ulaya wanaita tu wale ambao wako juu," anasema. Msomi wa Uingereza anaangazia kuwa katika nchi yake rejareja - pia inaitwa biashara ndogo ndogo - haiadhibiwi kwa kifungo, na kwamba hii ndio sababu "idadi ya wafungwa katika Amerika ya Kusini wengi ni wadogo sana kiumri kuliko ile ya Ulaya.

Image: GETTY IMAGES

Darke, kama Muñoz, anaamini kwamba sera hii ya kupambana na dawa za kulevya sio tu haina maana ("katika soko la usambazaji na uhitaji, kutakuwa na mtu mwingine aliye tayari kuuza", wanakubali), lakini kwamba pia ina athari.

"Haina tija kujaza magereza na watu ambao wanakamatwa wakiuza dawa kwa kiwango kidogo mitaani," anasema mwangalizi wa haki za binadamu wa HRW.

"Kuweka watu hawa, iwe kwenye kizuizi au kwa kutiwa hatiani, katika magereza ambayo yanadhibitiwa na vikundi vya wahalifu mwishowe hudhoofisha usalama wa Umma, kwa sababu watakuwa katika vyuo vikuu vya uhalifu halisi," anaelezea.

Magenge ya uhalifu

Katika kitabu chao "Prisons and Crime in Latin America", kilichochapishwa mwaka huu, wasomi Gustavo Fondevila na Marcelo Bergman wanaeleza kuwa magereza yametoka kuwa "vyombo vya kutoweza kufanya kazi, kuwazuia na kuwarekebisha waendelezaji wa vurugu na uhalifu".

Mapigano kati ya vikundi vya wahalifu wanaodhibiti magereza ndio yaliyosababisha mauaji ya wafungwa huko Ecuador, na machafuko ya hivi karibuni katika nchi nyingine kadhaa za eneo hilo, kama vile Peru, Venezuela na Brazil.

Wataalamu wanaonya kuwa msongamano una jukumu muhimu katika ukuaji wa magenge ya uhalifu. kwa sababu kuna udhibiti mdogo wa serikali," anasema Muñoz. Na anatoa mfano: "Ikiwa una seli ambayo ni ya watu watano, lakini kuna 30, walinzi hawawezi kudhibitI. Kwa hivyo msongamano unachochea ukuaji wa vikundi vya wahalifu."

Image: GETTY IMAGES

"Magereza ni jambo muhimu sana katika mitandao hii," anaongeza. "Kwa sababu wao ni waajiri." "Kwa kweli, katika ukanda huu tuna kesi nyingi za vikundi vya uhalifu ambavyo viliundwa katika magereza na kisha kufanya biashara haramu nje ya magereza," anaangazia, akitoa mfano wa shirika kubwa zaidi la uhalifu nchini Brazil(PCC) ).

Darke, kwa upande wake, anasema kuwa katika nchi nyingi maafisa wa magereza "wanahitaji magenge kupanga uendeshaji wa gereza." "Katika maeneo mengine magenge haya huteuliwa na mfumo wa magereza ili kuweka utulivu," anasema. Anaiita "serikali ya ushirikiano." "Wakati hautoi rasilimali kwa mfumo wa gereza na hauna wafanyakazi wanaohitajika, ni kawaida kwa watu wanaofanya kazi huko, na ambao hawawezi kusimamia gereza, kutafuta ushirikiano wa wafungwa," anaelezea .

Je! Ni suluhisho gani la kuzuia mnyororo huu mbaya, ambao, mbali na kuzuia uhalifu, unaendelea? "Lazima uwekeze katika kuzuia uhalifu, badala ya kuushughulikia uhalifu," anapendekeza Muñoz. "Ni mabadiliko katika mawazo ambayo yatakuwa ya msingi Amerika Kusini". Anaeleza Darke.