Dunia yetu inapoteza mwangaza', wanasayansi wasema

Image: GETTY IMAGES

Kwa miaka michache, dunia imekuwa ''ikipoteza mwangaza wake''

Hii inamaanisha, dunia yetu inarudisha mwangaza mdogo kutoka kwenye jua kuingia katika anga, kulingana na utafiti mpya uliochapishwa na jarida la Geophysical Research Letters la Muungano wa Wanajiografia wa Marekani (AGU) katika mwezi wa Septemba.

Waandishi wa utafiti huo, kutoka Marekani na Uhispania, waliafiki hili baada ya kuchanganua data juu ya kiasi cha mwangaza ambacho dunia inauonyesha kwa mwezi, ambao ulikusanywa kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita kwa kutumia setilaiti na kwa kutumia kifaa cha ufuatiliaji wa mienendo ya jua kilichopo mjini California.

Wanasayansi bado wana matumaini ya kutambua sababu za kupungua huku kwa mwangaza wa dunia, lakini tayari wana mawazo.

Hapa tunakwambia mawazo hayo ni yapi na ni athari zipi zinazoweza kutokea kwa sayari.

"Albedo" ni nini?

Kama inavyofahamika kuhusu mwangaza kwa ujumla, ni kwamba nyuso za mwangaza huojionyesha na nyuso nyeusi huufyonza mwangaza.

Kitu hicho hicho hutokea kwa mwangaza wa jua na dunia.

Maeneo ye ye mwangaza duniani kama yale ya kaskazini hutoa mwangaza dunian
Maeneo ye ye mwangaza duniani kama yale ya kaskazini hutoa mwangaza dunian
Image: GETTY IMAGES

Maeneo meusi ya sayari hufyonza mwangaza na joto kutoka kwa nyota yetu, huku maeneo ya mwangaza, kama vile nyuso za barafu za ncha na mawingu, huzionyesha na kuzirejesha kuelekea kwenye nafasi.

Kiwango cha mwanga kutoka kwenye jua ambacho kinapokelewa na dunia na kurejeshwa nyuma kinafahamika kama "albedo" na, kwa wastani, ni takriban 30% ya mwangaza wa jua unaopokelewa.

Kwa zaidi ya miaongo miwili. Kurejea huku kwa mwangaza au albedo kumekuwa kukipungua.

"Dunia sasa inaonyesha mwangaza wa chini ya watt kwa mita za mraba kuliko miaka 20 iliyopita. Hiyo ni sawa na kupungua kwa 0.5% wa mwangaza wa dunia ," unasema muungano wa AGU.

Kupungua huku kwa mwangaza wa dunia kumekuwa kukionekana zaidi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

"Kushuka kwa albedo kumekuja kama kitu cha kushangaza kwetu tulipoangalia data katika kipindi cha miaka mitatu baada ya miaka 17 ya kutokuwepo kwa albedo," anasema Philip Goode, mtafiti katika taasisi ya teknolojia ya New Jersey Institute , nchini Marekan, na mwandishi mkuu wa uchunguzi, akimaarisha data za mwangaza wa dunia kuanzia mwaka 1998 hadi 2017.

Lakini je upungufu huu unasababishwa na nini?

Sababu zinazowezekana

Waandishi wa utafiti hawakubaini mabadiliko katika mwangaza wa jua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kwahiyo kupungua katika mwangaza unaofikia dunia hakuhusiani na nyota, bali ni sababu za sayari yenyewe

Image: GETTY IMAGES

Sababu ambayo wanasayansi waligundua hapa dunaini ilikuwa na utofauti "mkubwa" katika kiwango cha mawingu katika baadhi ya maeneo ya bahari ya Pacific, alisema Enric Pallé, mmoja wa waandishi wa utafiti na mtafiti katika Instituto de Astrofísica de Canarias (IAC na kutoka idara ya fizikia ya nyota katika Chuo kikuu cha Laguna, nchini Uhispania, katika mahojiano idhaa ya BBC Mundo.

Kwa sasa kuna mawingu machache-na hivyo kusababisha kuwepo kwa nyuso chache za mwangaza unaong'ara-katika mashariki mwa bahari ya Pacific , kutoka kwenye mwambao wa Kaskazini na Kusini mwa Amerika , kulingana na data kutoka kwa mfumo 'unaofutilia mng'aro wa mawingu ya dunia- Earth-Cloud Radiant Energy System ( CERES), uliopo katika NASA.

Wanasayansi walihesabu mwanga kutoka katika jua ambao anaangaza katika mwezi
Wanasayansi walihesabu mwanga kutoka katika jua ambao anaangaza katika mwezi
Image: GETTY IMAGES

Athari

Wakati walipokuwa wakichunguza sababu za kupungua kwa mwangaza wa dunia, wanasayansi walibaini kwamba mwanga na joto kutoka kwa jua ambavyo dunia iliacha kuvipeleka hubakia katika sayari, katika bahari na katika hewa, kwahiyo, inaweza kuathiri viwango vya joto

"Kilicho wazi ni kwamba albedo ni kitu ambacho kilichukuliwa katika tafiti za hali ya hewa kama kitu fulani ambacho ni cha kudumu, lakini sio kwamba ni lazima tuendelee kupima kwasababu itataathiri pakubwa uwezo wetu wa kubashiri mabadiliko ya hali ya hewa baina ya sasa na miaka 20, 30 au 50 ijayo, "aliongeza kusema mwanasayansi Enric Pallé .

"Katika mienendo ya ongezeko la joto duniani kuna kupanda na kushuka kwa viwango vya joto," aliongeza mtafiti.

Kubaini kabisa utofauti ni upi katika albedo , "itatubidi tuendelee kupima kila mara jinsi sababu hizi zinabadilika katika miaka ijayo, kupima kwa muda mrefu ili kuona iwapo tunaweza kujihusisha kabisa katika mabadiliko ya tabia nchi au kuwa na uhakika kwamba hii sio tofauti asilia, "anasema Pallé.