Fahamu kwanini baadhi ya vifo vya ghafla hutokea wakati wa tendo la ndoa

Muhtasari

•Mwanaume anaweza kufia juu ya mwanamke, na mwanamke anaweza kufia chini ya mwanaume wakati wanapokuwa katika tendo la kujamiiana, jambo linalowashangaza wengi.

Image: MALAYALAMEMAGAZINE.COM

Tendo la ndoa hufurahisha, na kadiri wakati umeendelea kusonga tangu enzi za mababu zetu, ni tendo ambalo limetokea kufurahiwa na wanaume na wanawake.

Hatahivyo wale wanaofanya tendo la ndoa wanaweza kuwa katika hatari ya kufa kifo cha ghafla, au wote wanaweza kupata maambukizi au kuugua wakati wa tendo hilo.

Mwanaume anaweza kufia juu ya mwanamke, na mwanamke anaweza kufia chini ya mwanaume wakati wanapokuwa katika tendo la kujamiiana, jambo linalowashangaza wengi.

Kumekuwa na taarifa mbalimbali kwamba baadhi ya watu wamekufa kutokana na unyanyasaji wa kingono, jambo linalowashangaza wengi.

Huku baadhi wakisema ni hali ya kawaida ya kidunia, wengine mara kwa mara hulaumiwa kwa matukio hayo, hususan wale wanaoshiriki ngono nje ya ndoa.

Wengi huwa hawaamini tukio kama hili linapotokea.

Lakini wataalamu wa masuala ya tiba wameelezea mambo yanayoweza kusababisha mtu kufa wakati wa tendo hilo, iwe kwa wanawake au wanaume.

Yafuatayo ni mambo matatu yanayoweza kusababisha mtu kufa wakati wa kujamiiana.

1. Matumizi mabaya ya dawa:

Wanaume mara nyingi hutumia dawa za kitamaduni au miti shamba ili kuwasaidia kuwa thabiti wakati wa tendo hilo. Wengine huzichanganya na bia wakiamini kuwa zitawasaidia katika kuongeza nguvu za kiume na hivyo kuweza hata kujamiiana na wanawake zaidi ya mmoja.

Image: VIRALNIGERIA

Wakati mwingine, baadhi ya wanaume huvuta sigara, na madawa mengine ya mihadarati ili kuongeza nguvu zao za kiume. Hili halina ithibati ya kisayansi lakini ndio mambo ambayo watu hufanya .

Kile ambacho hawajui ni kwamba madawa hayo huwa na kemikali inayoitwa "Nitrate", ambayo inaweza kusababisha shinikizo la damu na kusababisha kifo cha ghafla wakati wa tendo hilo

Mwisho wa yote, athari zake huwa ni mbaya,licha ya heshima wanayoitaka kutoka kwa mwanamke wanayefanya naye tendo la ndoa

2. Maradhi ya moyo:

Matatizo ya kiafya sio jambo linalopaswa kupuuzwa inapokuja katika suala la kushiriki mapenzi

Mtu mwenye historia ya ugonjwa wa moyo anaweza kufa wakati wa tendo hilo kwasababu moyo wake utafanya kazi ngumu kuliko wakati wa kawaida

Sababu za mara kwa mara za magonjwa ya moyo, hususan kwa wanawake wenye zaidi ya miaka 50 na wanaume wenye miaka arobaini ni shinikizo la damu , uvutaji wa sigara, kisukari, kiharusi na magonjwa mengine.

Sababu nyingine ambayo mara nyingi husababisha magonjwa ya moyo ni msongo mkubwa wa mawazo.

Mshtuko wa moyo wakati wa tendo la ndoa mara nyingi unawakumba wanaume kuliko wanawake, utafiti unaonyesha.

Lakini tendo la ndoa ni kichocheo adimu cha mshutuko wa moyo .

Ni visa 34 tu vya mshtuko wa moyo kati ya 4,557 hutokea wakati au ndani ya saa moja ya kujamiiana na 32 ya wale walioathiriwa walikuwa wanaume.

Sumeet Chugh, wa Taasisi ya Moyo ya Cedars-Sinai Heart Institute alisema utafiti wake ni wa kwanza kutathmini shughuli za ngono kama sababu inayowezesha kusababisha mshutuko wa moyo.Utafiti wake huo ulichapishwa katika ripoti ya BBC Novemba mwaka wa 2017

Utafiti wake huo uliwasilishwa katika mkutano wa American Heart Association wakati wa kutathmini vichocheo vinavyosababisha mshtuko wa moyo .

Hatua hiyo hutokea wakati moyo unapopata matatizo na kuacha kupiga . Mtu hupoteza fahamu na kukosa kupumua Iwapo hatofanyiwa utaratibu wa CPR ili kumuokoa

Mshutuko wa moyo ni tofauti na shambulio ambalo hukumba moyo na kuzuia damu kuufikia .

3. Matumizi ya kupindukia ya dawa za kuongeza nguvu za kiume

Dawa ya Viagra imekuwa ikiuzwa katika maduka mbali mbali ya dawa duniani, kwa lengo la kuwasaidia wanaume hususan wenye magonjwa yaliyoathiri nguvu zao za kiume kuweza kurejesha uwezo huo.Kulingana na wataalamu dawa hii inapaswa kutolewa na Daktari kwa vipimo vinavyohitajika kulingana na tatizo lenyewe la kiafya.

Image: GETTY IMAGES

Hatahivyo kutokana na upatikanaji kwa njia rahisi wa dawa hizi, baadhi ya vijana na wanaume wamekuwa wakizinunua kiholela kwenye maduka ya dawa na kuzitumia ili kuwaridhisha wapenzi wao.

Kulingana na wataalam matumizi yasiofaa ya dawa hizi yanaweza kusababisha matatizo ya moyo na hivyo kuweza kuchochea kutokea kwa kifo wakati wa tendo hilo.