Je unazifahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa?

Muhtasari

• Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho nchini Korea Kaskazini.

Wanaharakati wanaounga mkono itumiaji wa bangi walionekana wakisheherekea uamuzi huo wa mahakama
Wanaharakati wanaounga mkono itumiaji wa bangi walionekana wakisheherekea uamuzi huo wa mahakama
Image: GETTY IMAGES

Lesotho

Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.

Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini

Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa.

Tangu mwezi machi mwaka 2017, baada ya mahakama kuu ya Western Cape kuhalalisha matumizi ya bangi majumbani bado matumizi yake ni kinyume cha sheria, mpaka pale sheria itakapobadilishwa kuruhusu wafanyabiashara walime na kuwekeza kwenye kilimo cha bangi, vivyo hivyo kwa makampuni kutengeneza bidhaa zitokanazo na bangi na mawakala kusambaza bidhaa.

katika kipindi cha miezi kadhaa nyuma, wale walioonyesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha bangi wameleta maendeleo makubwa kufungua milango katika uzalishaji wa bangi kwa ajili ya dawa.

Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi
Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi
Image: GETTY IMAGES

Ghana

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .

kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.

pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.

Korea Kaskazini

Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.