Kwanini ukosefu wa umeme nchini wa hivi karibuni umeibua maswali zaidi?

Kampuni hiyo imekuwa ikitumbukia katika shio la madeni. I

Muhtasari

•Maafisa wapya waliochukua uongozi wakiongozwa na Waziri Monica Juma na msaidizi wake Gordon Kihalangwa, wanaangaliwa na wengi kuwa watu wa Rais waliopewa Jukumu na Bw Uhuru Kenyatta kutekeleza mageuzi makali katika sekta hiyo, 

Image: KENGEN

Jumanne Kenya ilikumbwa na ukosefu wa umeme kote nchini, ambao ni mbaya zaidi kuwahi kushudia katika miaka ya hivi karibuni ambao uliliacha taifa gizani.

Ni ni mara ya tatu kwa taifa hilo kukosa umeme katika kipindi cha miaka minne, na suala hili limeibua maswali kuhusu uwezo wa ukiritimba wa msambazaji pekee wa umeme katika taifa hilo wa kampuni Kenya-Kenya Power and Lighting company wa kusambaza nishati hiyo katika taifa hilo bila kuyumba.

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo Jumanne, ililaumu ukosefu wa umeme (stima) kwa kuporomoka kwa nguzi za PYLONS zinazosaidia mfumo wa kiwango cha juu cha umeme unaounganisha mji wa Nairobi na bwawa la umeme la Kiambere lililopo Kati kati mwa Kenya.

Ukiritimba haukufichua kwa umma ni nini kilichosababisha kuanguka kwa minara hiyo ya umeme, lakini duru za ndani ya kampuni hiyo zilisema kuwa viashiria vya kwanza vilioonyesha uwezekano wa wizi wa miundo mbinu ya usambazaji wa umeme mjini Nairobi.

Hujuma au kushindwa?

Ukosefu wa umeme unakuja huku kukiwa na mabadiliko makubwa katika wizara ya nishati. Mwezi Septemba 2021, Rais uhuru Kenyatta aliwahamisha mawaziri wote Charles Keter na naibu wake Mhandisi Joseph Njoroge katika wizara ya nishati na kuwapeleka katika wizara nyingine katika mabadiliko ya baraza la mawaziri ambayo yalionekana kama jibu la changamoto ndani ya sekta hiyo ya nishati.

Maafisa wapya waliochukua uongozi wakiongozwa na Waziri Monica Juma na msaidizi wake Gordon Kihalangwa, wanaangaliwa na wengi kuwa watu wa Rais waliopewa Jukumu na Bw Uhuru Kenyatta kutekeleza mageuzi makali katika sekta hiyo, miongoni mwa mambo mengine,ikiwa ni pamoja na kupunguza garama ya umeme kwa asilimia 15 katika kipindi cha miezi mitatu.

Akiwa mbele ya tume ya bunge ya masuala ya umma, katibu mkuu wa wizara ya nishati Gordon Kihalangwa alionya kwamba kutakuwa na mabadiliko katika kampuni ya umeme ya Kenya ili kutoa fursa ya mageuzi.

Kihalangwa alisema kuwa hatua hiyo inaashiria kwamba uhalifu ulifanyika wakati makubaliano ya ununuzi wa nishati yalipoandaliwa.

Image: KENGEN

Vyanzo katika ndani ya wizara vinaashiria kuwa wakuu wa idara mbali mbali wamekuwa wakilazimishwa kujiuzulu huku wengine wakichagua kustaafu mapema ili kukwepa wimbi la mageuzi katika wizara hiyo linaloweza kuwatupa nje.

Kikosi kazi cha Rais juu ya mapatano ya ununuzi wa nishati kilipendekeza IPP ipunguze ushuru wao uliolipwa na Mmalaka ya umeme ya Kenya -Kenya Power kwa kiwango cha nusu ili kuambatana na viwango vya bei za kampuni ya KenGen.

Katika hatua ambazo zitaokoa mabilioni ya shilingi ya wanunuzi, kikosi kazi pia kitashauri kwamba mapatano yote ya ununuzi wa umeme ambayo kwa sasa yanasubiri kusainiwa yaahirishwe.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye gazeti la serikali ya tarehe 7 Januari, 2022, Wizara ya nishati ilithibitisha kwamba ilikwisha tekeleza punguzo la 15% la ushuru wa nishati ya umeme(stima).

Kupunguzwa kwa nishati na kuangaliwa upya kwa makubaliano ya ununuzi wa umeme huenda kulikata mbawa za baadhi ya watu katika wizara ambao hawajafurahia sana kuona mabadiliko hayo.

Ukiritimba unaohangaika

Kuanzia ukosefu wa mara kwa mara wa umeme na kucheleweshwa kwa juhusi za kurejeshwa kwa umeme, kuongezeka kwa garama za umeme na muda mrefu wa kuwaunganisha wateja wapya katika mfumo wa umeme wa taifa. Kenya Power imekuwa ikionyesha kuzorota katika utekelezaji wa majukumu yake.

Wakenya hawaridhishwi tena na malalamiko tu bali weamekuwa wakiipatia kampuni hiyo majina ya kejeli kama vile "Kenya Paraffin and Candles Limited" au kuikejeli kwa majina kama 'Mpango Wa Candle' wakati umeme unapotoweka.

Kampuni hiyo imekuwa ikitumbukia katika shio la madeni. Imejikuta ikiwa na madeni kutoka katika taasisi za kimataifa kama - Shirika la kimataifa la maendeleo (IDA), Benki ya uchina Exim Bank, na benki ya maendeleo ya Japan, yaliyodhaminiwa na serikali na kwahiyo kulipwa na serikali.

Taarifa kutoka ndani ya Kenya Power zinaonyesha kuwa kwa mikopo wa upangaji inachukua asilimia 48.4 ya Shilingi bilioni 109.96 za madeni iliyyokuwa nayo kufikia mwishoni mwa mwezi Juni mwaka jana, hii ikionyesha utegemezi wake wa deni katika kuendesha shuguli zake.

Makampuni husika yamekuwa katika sakata za kifedha zinazohusisha ununuzi. Ripoti ya awali ya ukaguzi, kwa mfano inaonyesha kuwa Kenya Power ilishikilia karibu vifaa vya thamani ya shilingi bilioni 9.8 , ikiwa ni pamoja na nyaya za umeme, mita , na transfoma ambazo zimekuwa katika hifadhi kwa zaidi ya miaka mitano, bila kutumika.

Kuhesabu hasara

Ukosefu wa umeme ulikuja baada ya Mamlaka ya usimamizi wa nishati na petroli (Epra) inataka kuwalipa wanunuzi kwa hasara ya fedha, uharibifu wa vifaa, kuumia mwili , na kifo kutokana na ukosefu wa umeme.

Kwa sasa, Kenya Power inalipa fidia kwa majeruhi na uharibifu wa vifaa vya umeme, lakini hailipi hasara za kifedha kwasababu ya kukata mawasiliano ya umeme.

Mapendezo ya sheria yataiwezesha Kenya ktumia mfumo unaotumiwa na nchi nyingi za Ulaya ambazo zinahitaji fidia za kukatwa kwa umeme kwa muda mrefu iwapo yatakuwa sheria.

Ingawa hasara ilitokea kutokana ukosefu wa umeme haijathamanishwa, biashara nyingi zinazotegemea umeme, vikiwemo viwanda na hata biashara ndogo kama vile maduka ya vifaa vya ujenzi na saluni zote zilihesabu hasara.

Mfanyabiasha, Sellah Anyango, anayefanya kazi katika saluni katika mji mkuu wa Nairobi aliimbia BBC matatizo yake.

''Biashara yangu inategemea kwa kiasi kikubwa umeme.

Nilikuwa na wateja wakija na kuondoka kwasababu hakukuwa na umeme. Biashara ilikuwa bado ilikuwa inazorota kutokana na janga la corona. Halafu hili? Tutalipaje kodi ya nyumba? Na mishahara kwa ukosefu huu wa umeme? Haikubaliki kabisa.''

Hatua ya kuelekea nishati ya jua

Makampuni makubwa vikiwemo viwanda vikubwa yanahamia katika mfumo wa nishati ya jua kwa kutafuta umeme wa kuaminika na wa bei nafuu pia yamelalamikia utendaji wa kampuni ya ugawaji umeme Kenya Power.