Maya Angelou: Mfahamu mwanamke wa kwanza mweusi kuonekana kwenye sarafu ya Marekani

Muhtasari

• Idara ya Hazina ilitangaza kwamba kwa heshima ya Angelou imetengeneza sarafu za senti 25, maarufu kama robo.

• Alizaliwa huko Missouri mnamo 1928 na akafa mnamo 2014, Angelou na kaka yake Bailey walipelekwa wakiwa watoto kuishi na nyanya yao katika mji wa Arkansas.

• Akiwa na umri wa miaka 7, alipotembelea Saint Louis, alibakwa na mpenzi wa mama yake.

Image: BBC/RON GROEPER

Mchangamfu na mwenye hekima, mwandishi na mshairi wa Kimarekani Maya Angelou alikuwa mfano wa kuigwa na ni mwanaharakati ambaye alijivunia kuwa mtu mweusi nchini Marekani.

Alikuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuandika na kukariri shairi wakati wa kuapishwa kwa rais wa Marekani mwenye asili ya Afrika - Bill Clinton mwaka 1993 - na sasa atakuwa wa kwanza kukumbukwa kwa sarafu.

Idara ya Hazina ilitangaza kwamba kwa heshima ya Angelou imetengeneza sarafu za senti 25, maarufu kama robo.

Hazina hiyo inapanga kutoa sarafu 20 zaidi za thamani hiyo katika kipindi cha miaka minne ijayo, zikiwakilisha wanawake wengine wa Marekani ambao walishiriki majukumu muhimu katika historia ya Marekani.

Maisha magumu ya utotoni

Alizaliwa huko Missouri mnamo 1928 na akafa mnamo 2014, Angelou na kaka yake Bailey walipelekwa wakiwa watoto kuishi na nyanya yao katika mji wa Arkansas.

Image: TESORO DE EE.UU.

Hivyo aliishia kuishi kwa takriban muongo mmoja katika mojawapo ya maeneo maskini zaidi nchini Marekani na kukumbana na ubaguzi wa rangi moja kwa moja katika eneo linaloitwa Deep South: maisha ambayo alikuja kusimulia kwenye sehemu ya kwanza ya wasifu wake uliochapishwa mnamo mwaka 1970.

Akiwa na umri wa miaka 7, alipotembelea Saint Louis, alibakwa na mpenzi wa mama yake. Baada ya kuiambia familia, mtu huyo alikamatwa, akahukumiwa na kuachiliwa kutoka gerezani, ingawa aliuawa muda mfupi baadaye.

Baada ya hilo, hakuzungumza tena kwa miaka mitano iliyofuata.

Taaluma isiyo ya kawaida

Ingawa hakuzungumza, alisoma sana, jambo ambalo lilifanya iwe rahisi kwa rafiki wa bibi yake ambaye alitambua mapenzi yake ya ushairi kumshawishi azungumze tena, akisema kwamba ili kufurahia kikamilifu, lazima aseme kwa sauti.

Angelou aliandika "Ninafahamu ni kwanini ndege wa pangoni huimba."
Angelou aliandika "Ninafahamu ni kwanini ndege wa pangoni huimba."
Image: BBC/WAYNE MILLER MAGNUM

Baadaye, alihama tena na mama yake hadi San Francisco, ambapo akiwa na umri wa miaka 15 akawa dereva wa kwanza wa gari la abiria katika jiji hilo.

Akiwa na umri wa miaka 16, alijifungua mtoto wake wa pekee, mvulana, baada ya mapenzi ya usiku mmoja aliyofanya kwa nia ya kufahamu.

Baada ya muda mfupi alikuwa ameanza taaluma isiyo ya kawaida ambayo ilijumuisha uchezaji densi na kahaba . Akawa mwigizaji na mwimbaji, akarekodi albamu ya nyimbo na kusafiri kwenda Ulaya katika shughuli za utengenezaji vipindi.

Katika safari yake ya maisha alipata wanaume wawili na akachukua jina lake la mwisho kutoka kwa mwanamume wa kwanza aliyekuwa mwanamuziki mtarajiwa wa Ugiriki kwa jina Enistasios Angelos.

Uanaharakati wa masuala ya kijamii

Mnamo 1961 alihudumu kwa muda kama mratibu wa Mkutano wa Martin Luther King. Kisha akamfuata mwanaharakati wa Afrika Kusini, Vusumzi Make, hadi Cairo, ambako alikuja kuwa mwandishi wa habari.

Baadaye akaenda nchini Ghana, ambako alikutana na mwanaharakati mweusi Malcolm X. Akarudi Marekani mnamo mwaka 1965 kufanya kazi naye, lakini aliuawa muda mfupi baadaye. Miaka michache baadaye Martin Luther King pia akauawa.

Angelou alizungumza mbele ya wajumbe katika usiku wa pili wa kongamano la kitaifa la chama cha democratic mwaka 2004
Angelou alizungumza mbele ya wajumbe katika usiku wa pili wa kongamano la kitaifa la chama cha democratic mwaka 2004
Image: REUTERS

"Mimi, pamoja na vijana kadhaa wakati huo, tulichukizwa, tulikasirika na kupinga ukosefu wa usawa," baadaye aliambia BBC alipokumbuka wakati wake na Martin Luther King na pia Malcolm X.

"Lakini hadi vuguvugu la haki za kiraia lilipojitokeza, hakukuwa na njia wazi ya kupinga ukosefu wa usawa," aliongeza.

Ilikuwa karibu wakati huu ambapo rafiki yake, mwandishi James Baldwin, alimsaidia kumshawishi aandike kitabu cha kwanza ya wasifu wake.

Kitabu hicho kilipata mauzo makubwa na vitabu sita zaidi vinafuata kwa miongo.

Alianza pia kuchapisha mashairi, akaandika mchezo wa filamu, akaandika na kutayarisha mfululizo wa vipindi 10 vya televisheni na utamaduni wa kiafrika wa Waameka weusi, na akaigiza kwenye mfululizo wa vipindi vya runinga vya Roots, kuhusu maisha ya utumwa.

Katika miaka ya 1980, alikua msomi na profesa wa masomo ya Amerika katika Chuo Kikuu cha Wake Forest huko North Carolina.

Kufikia wakati huo, labda alikuwa mwandishi mweusi aliyejulikana zaidi ulimwenguni na mmoja wa wanawake weusi wanaojulikana sana Amerika.

Bill Clinton alitambua hadhi yake alipomwomba asome shairi, lililoitwa "On the Pulse of the Morning," wakati wa kuapishwa kwake mwaka wa 1993.

Mnamo 2010, Barack Obama alimkabidhi Nishani ya Uhuru ya Rais, tuzo ya juu zaidi ya kiraia nchini Marekani.

Alipokea shahada kadhaa za heshima na akaandika zaidi ya vitabu 30 bora zaidi

Sarafu mpya inawakilisha Angelou kwa mikono iliyo wazi na iliyonyoshwa. Nyuma yake kuna ndege anayeruka na jua linalochomoza, ambayo "imechochewa na ushairi wake na kuashiria jinsi alivyoishi," Idara ya Hazina ya Marekani ilisema.

Upande mwingine wa sarafu unaonyesha sanamu ya George Washington, rais wa kwanza wa Marekani.