Afya ya akili: Hizi ndizo athari za kutazama picha za ngono

Muhtasari
  • Hizi ndizo athari za kutazama picha za ngono

Wanandoa wa Krishna-Mala (jina limebadilishwa) walikwenda kwa mtaalamu wa ngono kwa ushauri kuhusu kutoridhika ndani ya ndoa na matatizo ya kushika mimba. Uchunguzi ulionesha kwamba wote wawili hawakuwa na matatizo ya kimwili.

Mala baadaye alimwambia mtaalamu wa ngono kwamba mumewe alikuwa akitazama picha za ngono ponografia hadi saa nane usiku, walipoulizwa mmoja mmoja

Alisema hawezi kuzungumza na mtu yeyote kuhusu hilo kwa sababu alikuwa akiheshimika katika jamii yake. Jayarani Kamaraj, daktari wa uzazi na mtaalamu wa ngono, anasema mumewe Krishna alitibiwa kutokana na habari hii.

Anaeleza jinsi kutazama picha za ngono kunavyoweza kufanya kila mtu ahisi hivyo, kama ponografia inaweza kuhusishwa na elimu ya ngono, na jinsi ya kujua ikiwa mtu ana uraibu wa kutazama picha za ngono.

Kutazama picha za ngono ni jambo zuri au baya ?

Ponografia imegundulika kukithiri katika enzi ya corona na kwa wengi ni mtafaruku. Ponografia hutumiwa kwa aina fulani ya matibabu ya ngono.

Inaweza kuchukuliwa kama kichocheo kwa wale wanaokuja na matatizo ya kujamiana. Wanandoa huamua kutazama kwa ridhaa ya pande zote. Lakini ni hatari kwa watu chini ya umri wa miaka 18 kuona hili. Ponografia haiwezi kujumuishwa katika elimu ya ngono pia.

Ni aina gani ya matatizo ya afya ya akili yanayoweza kusababishwa na kutazama picha za ngono?

Tafiti zinaonesha kwamba kutazama ponografia pekee kunapunguza msongo wa mawazo na kuchanganyikiwa. Lakini, mara kwa mara kuangalia ponografia, hiyo yenyewe ina matokeo mabaya.

Huongeza msongo na kuchanganyikiwa. Ponografia kupita kiasi inaweza kusababisha matatizo katika ndoa. Kukatishwa tamaa hutokea kati ya wanandoa wakati akili inapoanza kutarajia mifumo ya kufikirika, isiyowezekana ya ngono.

Namna gani utaweza kubaini kuwa mtu ana uraibu wa kutazama picha za ngono?

Watu wanaotazama picha za ngono wanaweza kugawanywa katika makundi matatu. Kutazama ponografia kwa dakika 17 hadi 24 tu kwa juma kunaonwa kuwa hakuna madhara. Uchunguzi unaonesha kuwa karibu 75% ya watu ni wa jamii hii. Hawana matatizo yoyote ya kifamilia wala kiakili.

Kwa wale ambao ni wa kundi la pili, kutazama ponografia kwa muda mfupi ni jambo la uzito na la kulazimisha. Wana nia ya kuiona tena na tena. tafiti zinaonesha kuwa wanaunda takriban asilimia 13 ya idadi ya watu.

Takriban asilimia 11 ni wa kundi la tatu. Wanatumia zaidi ya dakika 110 kwa wiki kutazama ponografia. Wana matatizo mengi kama vile palpitations, hasira, kuwashwa na upweke. Wanaume wengi hawana maradhi ya asubuhi.

Wanaotazama picha za ngono wanahitaji matibabu?

Inahitajika kwa hakika. Wanaume na wanawake wanaotazama ponografia kwa wingi hugunduliwa kuwa na matatizo ya ubongo. Kupoteza kumbukumbu, kukosa usingizi, matatizo ya utambuzi, na kutojali hutokea. Hawa wanahitaji kutibiwa.