Wanawake wenye ushawishi wanaodhibiti siasa za Mt. Kenya

Muhtasari
  • Orodha ya wanawake wenye nguvu wanaodhibiti siasa za Mlima Kenya
CHEGE
CHEGE

Katika muda wa miezi michache iliyopita, eneo la Mlima Kenya limekuwa kitovu cha shughuli zote kuu za kisiasa nchini.

Huku siasa za 2022 zikiwadia, makundi mawili ya kisiasa yameibuka na wanasiasa wa kike katikati mwa michezo ya kugombea madaraka katika eneo hilo.

Kwa hivyo, ni akina nani hawa wanawake wanaothubutu kupambana koo na  wenzao wa kiume?

1.Martha Karua

Yeye hata hahitaji utambulisho wowote Maisha yake ya kisiasa yanachukua zaidi ya miongo mitatu. Akijulikana na wengi kama 'Iron Lady', Karua aliwakilisha eneo bunge la Gichugu kwa mihula minne bila kukatizwa kuanzia 1992 hadi 2013. Pia alihudumu katika Baraza la Mawaziri kwa miaka 6.

Ingawa hana nafasi yoyote ya kuchaguliwa baada ya azma yake ya kushindwa kuwania kiti cha Ugavana wa Kirinyaga, sauti ya Karua ya kisiasa inaheshimiwa kote nchini. Anapozungumza, watu husikiliza.

2.Anne Waiguru

Ni mwanasiasa ambaye amekuwa katika ulingo wa siasa kwa muda huku hata licha ya kupokea kejeli nyingi sauti yake ya siasa inafahamika mlima Kenya.

3.Sabina Chege

Tangu kuchaguliwa kwake kama Mwakilishi wa Wanawake wa Murang'a mnamo 2013, Sabina Chege amekuwa mmoja wa watu wanaotambulika kisiasa katika eneo hili. Huku akionekana na wengi kama mwanasiasa mwenye akili timamu nchini, amekuwa mstari wa mbele kumtetea Rais Uhuru Kenyatta.

4.Alice Wahome

Katika siku chache zilizopita, jina lake limekuwa likivuma katika duru za kisiasa. Kwa nini? Kwa sababu alimchukua Rais ana kwa ana huku kukiwa na madai kwamba anapanga kugombea kiti kingine cha kisiasa mwishoni mwa muhula wake.