Fahamu jinsi matumizi ya bangi yanavyoathiri bangi

Muhtasari

•Utumiaji wa bangi unaweza kuathiri mfumo wa utambuzi, tafiti zinasema, haswa kwa wale wanao utumiaji kwa wingi.

Image: BBC

Mmea wa bangi umekuwa ukitumiwa na binadamu kwa zaidi ya miaka elfu moja.

Ingawa inajulikana zaidi kwa matumizi yake kama burudani ambayo inavutwa au kumezwa, pia imehalalishwa kwa matumizi ya dawa za matibabu katika nchi mbalimbali duniani.

Lakini inaathiri vipi akili zetu?

Tatifi tatu za zilizochapishwa na majarida ya Psychopharmacology, jarida la Neuropsychopharmacology, na International Journal of Neuropsychopharmacology inaonesha jinsi matumizi yake yanavyoweza kuathiri hatua za utambuzi na kisaikolojia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Dawa na Uhalifu liliripoti kuwa takriban watu milioni 192 duniani kote kati ya umri wa miaka 15 na 64 wanatumia bangi kwa burudani, kulingana na takwimu za 2018.

Na karibu 35% ya watumiaji hawa wana umri wa kati ya miaka 18 na 25.

Hii inaonyesha kuwa watumiaji wengi ni vijana, ambao akili zao bado zinaendelea kukua, jambo ambalo linaweza kuwafanya kupata athari zaidi katika ubongo zinazohusishwa na matumizi ya muda mrefu ya bangi.

Tetrahydrocannabinol ndio kiungo kikuu kinachoathiri ubongo katika bangi na eneo linalokwenda kuathiri ni katika mfumo wa endocannabinoid, ambapo kuna vipokezi vinavyoguswa na kemikali vya jani hili.

Uwepo wa vipokezi hivi ni umuhimu katika maeneo ya awali na ya viungo vya ubongo, .

Hudhibiti dopamini, asidi ya gamma-aminobutyric, na uashiriaji wa glutamati kwenye ubongo.

Hiyo ina maana gani? Tunajua kwamba dopamine inahusika katika kuhisi, kujifunza na kutambua na kumbukumbu.

Ingawa asidi ya glutamate na gamma-aminobutyric zina kazi katika mchakato wa utambuzi, ikiwa ni pamoja na kumbukumbu na kujifunza.

Athari za Kutambua

Utumiaji wa bangi unaweza kuathiri mfumo wa utambuzi, tafiti zinasema, haswa kwa wale wanao utumiaji kwa wingi.

Hiyo ni, watu wenye hamu ya kutumia mara kwa mara na kuharibu shughuli zao za kila siku kama vile kazi au kusoma.

Inakadiriwa kuwa 10% ya watumiaji wa bangi hukutana na tatizo la ugonjwa wa utambuzi.

Katika utafiti wetu, tulifanikiwa kupima takriban watu 39 wenye ugonjwa huu (ilibidi wawe 'safi' siku ya upimaji) na tukalinganisha na watu 20 ambao hawakuwahi kutumia bangi au mara chache sana.

"Tuliweza kuonyesha kwamba washiriki waliokuwa na tatizo hilo walikuwa na utendaji mbaya zaidi wa kazi katika majaribio ya kumbukumbu Cambridge Neuropsychological Test (jaribio lililoundwa kutathmini uwezo wa ubongo wa kuhifadhi kumbukumbu), ikilinganishwa na wengine ambao hawakuwahi au hutumia mara chache sana".

Utumiaji pia umeonyeshwa kuwa na athari mbaya katika "utendaji wa kazi," ambazo ni hatua ya ubongo inayojumuisha fikra nyepesi.

Athari hii inaonekana kuwa inahusiana na umri ambao matumizi ya madawa huanza: kwa wenye umri mdogo, utendaji wa utendaji zaidi huathiriwa.

Uharibifu katika mfumo wa utambuzi pia umegunduliwa kwa watumiaji wa mara chache. Kundi hili huwa hufanya maamuzi hatari zaidi kuliko wengine na lina matatizo zaidi ya kupanga.

Ingawa tafiti nyingi zimefanywa kwa wanaume, kuna ushahidi wa tofauti ya athari katika jinsia tofauti.

Tumeonyesha kuwa ingawa watumiaji wanaume wana kumbukumbu duni na ugumu wa kutambua vitu, wanawake wanaotumia bangi wana matatizo ya umakini zaidi na matatizo ya utendaji katika kazi.

Tofauti hizi zinaendelea wakati tafiti zinafanywa kwa kuzingatia umri, IQ, matumizi ya pombe na nikotini, dalili za hisia na wasiwasi, utulivu wa kihisia na tabia.

Image: BBC

Kuhisi na afya ya akili

Matumizi ya bangi pia huathiri jinsi tunavyohisi, na pia kuathiri jinsi tunavyofikiri.

Kwa mfano, baadhi ya utafiti wa awali unaonyesha kwamba kuhisi na kufikiri—pamoja na mizunguko ya ubongo inayohusika katika hatua hii—huweza kuathiriwa tunapotumia bangi.

Hili linaweza kuathiri utendaji wetu shuleni au kazini, na linaweza kutufanya tuhisi kuwa na ari ya kufanya kazi na kutopata thawabu tunapofanya vyema.

Katika utafiti wetu wa hivi karibuni, tulitumia kazi ya kufikirika, ambapo washiriki walipitishwa kwenye skana ambapo waliona miraba ya rangi ya bluu na machungwa.

Miraba ya rangi ya chungwa huleta zawadi ya pesa ikiwa mshiriki angejibu.

Muundo huu ulitusaidia kuchunguza jinsi ubongo hujibu anapopata zawadi

Tunazingatia hasa striatum ya tumbo, ambayo ni eneo muhimu katika mfumo wa kuhisi wa ubongo.

Tulibaini kuwa athari kwenye mfumo wa hisia zilikuwa za hila, na athari za moja kwa moja za bangi kwenye striatum ya ventral.

Hata hivyo, washiriki katika utafiti wetu walikuwa watumiaji wa wastani wa bangi. Madhara yanaweza kujulikana zaidi kwa watumiaji wa muda mrefu.

Pia kuna ushahidi kwamba bangi inaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili.

Tumeripoti kuwa inahusiana na anhedonia ya juu, ambayo ni kutokuwa na uwezo wa kusikia raha, kwa vijana.

Matatizo ya kisaikolojia

Athari hii pia ilionekana mara kwa mara wakati wa marufuku ya kutoka nje kutoikana na janga la covid-19.

Matumizi ya bangi kwa vijana pia yametajwa kuwa sababu ya kuendelea kwa matukio ya kisaikolojia, pamoja na schizophrenia.

Utafiti mmoja unaonyesha kwamba matumizi ya wastani ya bangi huongeza hatari ya dalili za kisaikolojia kwa vijana, lakini ina athari kubwa kwa wale walio na mwelekeo wa kisaikolojia (alama za juu kwenye dalili za paranoid na psychoticism).

Hatujui kwa nini bangi inahusishwa na matukio ya kisaikolojia, lakini nadharia kadhaa zinaonyesha kuwa dopamine na glutamate zinaweza kuwa muhimu katika neurobiolojia ya hali hizi.

Utafiti mwingine wa vijana 780 unapendekeza kwamba uhusiano kati ya matumizi ya bangi na uzoefu wa kisaikolojia unahusishwa na eneo la ubongo linaloitwa "uncus."

Hii iko ndani ya parahippocampus (inayohusika katika kumbukumbu) na balbu ya kunusa (inayohusika katika mchakato wa kusikia harufu), na ina idadi kubwa ya vipokezi vya cannabinoid.

Hatimaye, athari za kiakili na kisaikolojia za matumizi ya bangi zinaonekana kutegmeana kwa kiasi fulani katika kipimo cha (Uhuru, muda, na uwezo), jinsia, udhaifu wa kijenitiki, na umri wa kuanza.

Lakini tunahitaji kuamua ikiwa athari hizi ni za muda au za kudumu. Makala yenye muhtasari wa tafiti nyingi imependekeza kuwa, kwa matumizi ya wastani ya bangi, athari zinaweza kudhoofika baada ya vipindi vya kujizuia kutumia.

Lakini licha ya hivyo inafaa kuzingatia madhara ya matumizi ya muda mrefu yanaweza kuwa kwenye akili zetu, hasa kwa vijana ambao akili zao bado zinaendelea kukua.

* Makala haya yameandikwa na Barbara Jacquelyn Sahakian anayeshughulikia masuala ya afya ya akili na uharibifu wa mfumo wa neva kutoka NIHR Cambridge Biomedical Research Center (BRC) na NIHR MedTech na In Vitro Diagnostic Cooperative (MIC), pamoja na watafiti Christelle Langley, Martine Skumlie na Tianye Jia .