Watu weusi ni wapweke zaidi duniani kuliko wengine-Utafiti mpya

Muhtasari
  • Watu weusi wana uwezekano mkubwa wa kujiskia upweke kuliko watu wengine kwa ujumla, kwa mujibu wa utafiti mpya
stress (1)
stress (1)

Watu weusi wana uwezekano mkubwa wa kujiskia upweke kuliko watu wengine kwa ujumla, kwa mujibu wa utafiti mpya.

Takwimu kutoka kwa Taasisi ya masuala ya Afya ya Akili (Mental Health Foundation) zinaonyesha kuwa mtu mmoja kati ya watatu weusi amewahi kukumbwa na hisia za upweke.

Hiyo inalinganishwa na idadi ya watu kwa ujumla ambapo mtu mmoja kati ya wanne alikuwa ameripoti upweke wakati fulani wa maisha yake au wakati wote. Mmoja kati ya watu watatu wenye umri wa miaka 16-24 pia walisema wanapata upweke.

Msemaji wa taasisi hiyo anasema ubaguzi wa rangi na usawa wa kijamii vinaweza kuchangia viwango hivi vya juu. Taasisi hiyo ilichunguza watu 6,000 kote Uingereza.

Hisia za aibu'

Rhyanna anasema alitambua kuwa alikuwa mpweke baada ya kujifungua mtoto wake wa kiume alipokuwa na umri wa miaka 17. Amekuwa akizungumza na podikasti ya Radio 1Xtra kupitia BBC inayoitwa If You Don't Know.

"Nilihisi hali ya kuwa mpweke zaidi kila wakati," anasema.

Hakuwa ametengwa, bali alijihisi upweke."Ni aibu kidogo ... unahisi kama uko peke yako lakini una watu hawa wote karibu nawe.

"Kwa nje, ni hisia ya aibu kwa sababu ninajitenga dhidi ya wazo hili la kuwa mtu hodari, mvumilivu, anayedumu ambaye nimejiengea tabia yangu."

'Weka wazi au nyamaza'

Anasema pia aliona vigumu kueleza hisia zake kwa sababu ya kuwa mweusi.

"Kulazimika kukubali kwamba - kama mwanamke mweusi mwenye nguvu - inaweza kuwa kitu ambacho hutaki kukubali katika jamii zetu kwa sababu unataka kuendelea," Rhyanna, ambaye ana umri wa miaka 32, anaongeza.

"Ndani ya jamii yetu ukipatwa na tatizo hulizungumzii, katika familia yangu ama usema ama unyamaze... sivyo nilivyotaka kuishi maisha yangu.

"Nilitaka kuzungumza juu ya uzoefu wangu kwa sababu ina maana kwamba wengine wanaweza kuzungumza juu yao pia."

Rhyanna hayuko peke yake - kulingana na Mental Health Foundation, robo ya watu wazima wa Uingereza wamewamewahi kuhisi wapweke wakati fulani au wakati wote, katika mwezi uliopita.

Kutengwa na upweke ni vitu viwili tofauti," Marwah El-Murad, kutoka Shirika la Afya ya Akili, anaiambia podcast.

"Unaweza kutengwa, usiwe na muingiliano na wengi ama mengi katika maisha yako na usijisikie mpweke - unaweza kufurahia hali hiyo.

"Vile vile unaweza kuwa mtu ambaye una marafiki wengi, familia kubwa... hupati kamwe kuwa peke yako lakini bado unaweza kuwa mpweke katika mazingira hayo."

Kwa hivyo kwa nini watu wengi weusi wanaripoti kuwa wapweke kuliko idadi ya watu kwa ujumla? Hii inaweza kuwa ni kwa sababu ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi mwingine.

'Upweke unaweza kutokea kwa mtu yeyote'

Taasisi hiyo ya hisani linaitaka serikali kuwekeza tena katika huduma za vijana. Takwimu zilizotolewa mwaka jana zinaonyesha ufadhili wa baraza kwa huduma za vijana huko London ulipunguzwa kwa nusu katika miaka 10 tangu ghasia za London mnamo 2011.

Anza na wewe mwenyewe'

Rhyanna ana ushauri ikiwa unakabiliwa na upweke kwa mara ya kwanza. "Anza na wewe mwenyewe kujiuliza kwa nini unahisi upweke. Je! ni kitu gani unachohisi kinakuzuia au kukuzuia kuwa kijamii? Je! ni kitu kinachohitaji kubadilika katika mitandao yako ya kijamii na mzunguko wa kijamii?

Ukiweza kulifanyia kazi hilo, anasema, unaweza kupata mabadiliko chanya katika maisha yako. Vidokezo vingine vilivyopendekezwa katika podikasti, kwa watu wanaohisi upweke, ni pamoja na:

  • Zungumza usikae kimya, uzungumze na mtu - rafiki, mfanyakazi mwenzako, daktari wako au simu ya msaada
  • Jip[ende kwa ukarimu - jipe ​​mapumziko na ufanye kitu unachopenda
  • Ungana na jumuiya yako - labda jaribu kwenda kwenye uwanja wa michezo, jiunge na klabu au mtu wa kujitolea
  • Jaribu kutojilinganisha na wengine