Wakazi walalamika baada ya wapenzi kugeuza kichaka kuwa madanguro Migori

Muhtasari

•Wakazi wanasema sauti za kufanya mapenzi , mipira ya kondomu iliyotumika na nguo za ndani to zilizoachwa imekuwa mambo ya kawaida.  

•Wakazi walisema  akina mama wa nyumbani au wanandoa wasio waaminifu wanaoogopa kukamatwa kwenye nyumba za wageni  ndiposa wanapendelea msitu

Muonekano wa angani wa mji wa Migori.
Muonekano wa angani wa mji wa Migori.
Image: MANUEL ODENY

Wakaazi wa mji  wa Oruba,Kauti ya Migori wanalalamikia kuwekwa katika mazingira yasiyo na starehe na wanandoa waliogeuza kichaka kuwa eneo la mapenzi.

Watu wanaoishi karibu na Kamarienga wamesema kuona wapenzi wakishikana mikono na kukumbatiana kisha  kutoweka kwenye vichaka kumewaletea usumbufu mkubwa.

Watoto kutoka shule za karibu na wafanyabiashara wanaoelekea katika soko la mji wa Migori walisema sauti za kufanya mapenzi , mipira ya kondomu iliyotumika na nguo za ndani to zilizoachwa imekuwa mambo ya kawaida. 

“Tunafahamu malalamiko hayo. Tunasikitishwa kwamba watoto wanaosoma shule wamepatikana wakicheza na kondomu, wakizungumza na kuiga walichokiona vichakani,” chifu wa Suna Oruba Charles Ouma alisema.

 Ouma alisema miezi kadhaa iliyopita, walipokea malalamishi sawa na hayo. Kwa pamoja na Nyumba Kumi, walianza doria na hali ikadhibitiwa. Walakini, ilianza tena hivi majuzi.

 "Hapo awali, tulikamata wahalifu kadhaa, wengine walikamatwa huku wengine wakifukuzwa," chifu alisema.

Alisema kichaka hicho kipo katika eneo lenye kinamasi, ambalo halina watu wengi na mara kwa mara hutumika kama eneo la kutupia taka ambalo limewavutia wanandoa hao. 

“Wamekuwa wakiharibu miti na vichaka, mbali na kuleta usumbufu. Wazee wako machoni na watakaopatikana watafikishwa mahakamani,” Ouma alisema. 

Mkazi Anna Adhiambo alisema wakati mashamba mengine katika mji wa Migori yana nyumba za kulala wageni, Oruba inajulikana kwa ukosefu wa usalama jambo ambalo limewatia hofu wawekezaji. 

"Unapopita na kuona mwanamume na mwanamke wakirandaranda, tunaondoka kabla hawajatoweka," Adhiambo alisema. 

Wakazi walisema akina mama wa nyumbani au wanandoa wasio waaminifu wanaoogopa kukamatwa kwenye nyumba za wageni  ndiposa wanapendelea msitu kwa sababu ni wa bei nafuu na labda hutoa mandhari ya asili ya kufanya mapenzi badala ya mpangilio wa kawaida wa vyumba vya kulala.

Hili pia, limeambatana na gharama ya juu ya maisha kwani gharama ya makaazi ya bei nafuu imepanda kutoka Sh300 hadi Sh500 katika mji wa Migori.

 "Tuna nyumba nyingi za kulala wageni katika mji wa Migori na hatutaruhusu eneo letu kuwa la aibu, tutawakamata watu kadhaa ili kutuma ujumbe," Ouma alisema.