Wafahamu magaidi watano wakuu wanaosakwa zaidi duniani

Muhtasari

•Hawa ni watu watano waliojificha nchini Somalia, baada ya kuwekwa katika orodha ya majasusi wa kimataifa.

Image: GETTY IMAGES

Tangu kuvunjika kwa serikali kuu ya Somalia, nchi hiyo imekuwa na idadi kubwa ya watu wakimbizi wa ndani. Miongoni mwao ni baadhi ya watu wanaoshukiwa kufanya mashambulizi katika balozi za Marekani.

Hawa ni watu watano waliojificha nchini Somalia, baada ya kuwekwa katika orodha ya majasusi wa kimataifa.

Fasul Abdalla

Fasul Abdalla alikuwa ni mmoja wa watu waliosakwa zaidi ambaye aliuawa katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Marekani imemshutumu kuhusika na mashambulio ya ugaidi ya mwaka 1998 dhidi ya balozi zake za Tanzania na Kenya.

Pia alidhaniwa kuwa ndiye aliyekuwa nyuma ya msururu wa mashambulio yaliyofanyika katika Hoteli maarufu ya Paradise Hotel iliyopo Mombasa Kenya na shambulizi la kombora dhidi ya ndege ya Israeli mwaka 2002.

Fasul alizaliwa katika visiwa vya Comoro katika miaka ya 1970. Anasemekana aliwahi kuishi katika nchi ya Saudi Arabia wakati alipokuwa mwanafunzi.

Abu-Mansur Al-Amriki

Omar Hammami, al maarufu Amriki, aliwasili nchini Somalia mwaka 2006, na kuwa mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa kundi la al-Shabaab.

Image: BBC

Alikulia katika eneo la Daphne, Alabama, nchini Marekani. Kulingana na watu waliosoma naye. Alikuwa mwanafunzi mkakamavu, na wakati mmoja aliwahi kuchaguliwa kuwa kiongozi wa wanafunzi.

Anaaminiwa kuuawa Somalia katika mwaka 2013, kufuatia mzozo katika kundi lake la al-shaabab

Samantha Lewthwaite 'White Garden'

Mtoro wa muda mrefu amekuwa nchini somalia kwa miaka saba

Anaripotiwa kutoroka Somalia baada ya kutalikiana na mume wake msomali, kulingana na baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya na Uingereza.

Samantha Lewthwaite
Samantha Lewthwaite
Image: BBC

Alik uwa ni mmoja wa magaidi wanaosakwa sana duniani, na alifahamika kote duniani kama White Widow. Samantha, ambaye ni raia wa Uingereza, anasemekana alikuwa mmoja wa zaidi ya wanawake 200 waliopo katika ujasusi wa al-Shabaab , kulingana na vyombo vya habari vya kimataifa.

Liban alijiunga na al-Shabaab katika mwaka 2006
Liban alijiunga na al-Shabaab katika mwaka 2006
Image: FBI

Liban Haji Mohamed na raia wa Marekani mwenye asili ya Kisomali. Aliishi katika jimbo la kaskazini mwa Virginia nchini Marekani . hatahivyo mwaka 2006 alienda nchini Somalia kujiunga na al-Shabaab.

Anashutumiwa kwa kutoa usaidizi wa kijeshi kwa al-shaabab, ambapo mahakama ya kijimbo ilitoa waranti ya kukamatwa kwake.

Shirika la ujasusi la Marekani FBI limetangaza zawadi ya dola 50,000 kwa atakayepelekea kumatwa kwake.

Badri walikuwa pamoja na mwanaume mwingine kwa jina salah, ambaye anasakwa na Marekani
Badri walikuwa pamoja na mwanaume mwingine kwa jina salah, ambaye anasakwa na Marekani
Image: BBC

Badri Abdicasiis

Badri ni Msomali kutoka Kenya. Kesi yake ni tofauti na wajumbe wengine waliotajwa awali ambao walishitakiwa kwa ugaidi. Anashitakiwa kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya na pembe za ndovu.

Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi ulituma picha yake na ilisambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, na zawadi ya dola milioni 1 inatarajiwa kutolewa kwa atakayepelekea kukamatwa kwake.

Badri alikamatwa katika eneo la Liboi, katika kaunti ya Garissa County alipokuwa njiani kuelekea nchini somalia, katika kituo cha kupambana na ugaidi. Anaaminiwa kukamatwa alipokuwa akijiandaa kutoroka kuelekea nchini somalia.

Abdi Hussein Ahmed, ambaye anaaminiwa kumtorosha Badri, pia anatafutwa. Kiasi cha dola milioni moja kimetangazwa kutolewa kama zawadi kwa yeyote atakayetoa taarifa kumuhusu. Inaaminiwa kuwa alionekana mara ya mwisho kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.