Fahamu kwa nini mwanamke na mwanaume hawapaswi kufanya mazoezi pamoja

Muhtasari

•Uchunguzi unaonyesha kuwa wanawake hupoteza mafuta mengi wakati wa kufanya mazoezi asubuhi, wakati wanaume hupoteza uzito zaidi wakati wa kufanya mazoezi jion

•Kulingana na watafiti, wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuchoma mafuta asubuhi kwa sababu ya mafuta mengi huwa kwenye tumbo.

Mazoezi ya asubuhi ya mapema yanatajwa kuwa ni muhimu na yenye afya kwa wanawake wanaotaka kupunguza uzito na kupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa nchini Marekani, mazoezi ya viungo ni mazuri kwa afya yako bila kujali muda wa siku unaofanya, lakini muda wa kufanya mazoezi katika siku husika na kupata matokeo mazuri hutofautiana kati ya wanaume na wanawake.

Uchunguzi unaonyesha kuwa wanawake hupoteza mafuta mengi wakati wa kufanya mazoezi asubuhi, wakati wanaume hupoteza uzito zaidi wakati wa kufanya mazoezi jioni.Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya kisayansi yaliyotokana na wanaume na wanawake walioshiriki katika utafiti huo, kwa mujibu wa watafiti waliofanya utafiti huo.

Utofauti wa homoni, nguvu za kimwili na usingizi kwa wanawake na wanaume zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye hili.Utafiti huo uliohusisha wanaume 30 na wanawake 26 - wote wakiwa timamu na wenye afya njema na umri kati ya miaka 25 na 55 - ulidumu kwa wiki 12 na kufuatilia matokeo ya aina tofauti za mazoezi.

Kundi moja la washiriki katika utafiti walifanya mazoezi kwa saa moja kabla ya 2:30 asubuhi, wakati wengine walifanya mazoezi yanayolingana jioni, kati ya 12 na saa 2 usiku, makundi haya yote yalifuata ratiba maalum ya chakula.

Mazoezi sasa au baadae?

Image: GETTY IMAGES

Watafiti walijaribu kuangalia shinikizo la damu la kila mtu na mafuta ya mwili wakati wa utafiti, pamoja na shughuli zao mwanzoni na mwisho wa utafiti. Washiriki wote katika utafiti waliboresha afya na shughuli zao wakati wa jaribio la wiki 12, bila kujali muda wao wa mazoezi.

"Wakati mzuri wa kufanya mazoezi ni wakati unapoweza na kufanya ratiba yako iwezekane," Dk. Paul Arcerio, mtafiti mkuu na mhadhiri katika Chuo cha Skidmore, New York.Lakini anapendekeza kwamba kuna sababu nyingine: wakati mzuri wa kufanya mazoezi wakati wa mchana ni tofauti kwa wanawake na wanaume.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo, wanawake wanaotaka kupunguza kiuno na kupunguza shinikizo la damu wanatakiwa kufanya mazoezi asubuhi, kwa mujibu wa Dk. Arcer. Hii ni muhimu kwa sababu mafuta yaliyoko katika eneo la kiuno au tumbo la chini yako karibu na viungo muhimu vya mwili, ikiwa ni pamoja na ini, na hiyo inaweza kuwa hatari.

Kinyume chake, alisema, wanawake wanaotaka kujenga misuli na afya kwa ujumla wanapaswa kufanya mazoezi jioni. Wanaume ambao walifanya vipimo mara nyingi hawakuwa wanaathiri muda wa mazoezi, kwani afya na nguvu zao ziliendelea kuwa bora asubuhi na jioni.

Lakini mazoezi ya jioni yanasemekana kuwa "mazuri kwa wanaume wanaotaka kuboresha afya ya moyo, pamoja na hali yao ya kiakili," kulingana na Dk. Arcerio.Kuboresha afya ya mwili ni pamoja na kupunguza hatari ya magonjwa kama vile unene wa kupitiliza, kisukari cha aina ya 2, ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Haijulikani kwa hakika kwa nini nyakati za mazoezi ni tofauti kwa wanaume na wanawake, na watafiti wanasema mengi zaidi yanahitajika kufanywa. Kulingana na watafiti, wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuchoma mafuta asubuhi kwa sababu ya mafuta mengi kwenye tumbo.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Frontiers in Physiology, ulifanywa kwa watu wanene, lakini watafiti walisema kipimo hicho kilichoelezwa awali kinaweza pia kufanywa kwa watu wanene.

"Wanaweza kuwa na manufaa sana," alisema. Arcerio.