Wajackoyah afichua sababu za kuvalia durag kichwani

Muhtasari

•Tume ya IEBC ilimdhinisha Wajackoyah kuwania kiti cha urais pamoja na mgombea mwenza wake Justina Wamae.

•Durag ni kitambaa kinachositiri kichwa ambacho hufungwa ili kuikinga nywele .

Mgombea urais wa Roots Party George Wajackoyah
Mgombea urais wa Roots Party George Wajackoyah
Image: EZEKIEL AMING'A

Mgombea rais kwa ticketi ya Roots Party of Kenya  Prof. George Wajackoyah amefichua kwamba huwa  anatumia durag kama ishara ya kupingana na  ufisadi nchini Kenya.

Akiwa kwenye mahojiano na runinga ya Citizen tv,Wajackoyah alizungumza kuhusu maisha yake ya kawaida ya awali.

“Nilikuwa chokora na mchimba  makaburi,alisema.

‘ Niko na watoto na bibi ambao wanaishi Merekani, durag ni ishara ya kupigana na ufisadi. Wakati Wamarekani wenye asili ya Kiafrika walikamatwa na kufungwa,wengi wao walikufa wakiwa kwenye  mashua ,mili yao ilitupwa baharini. Kabla ya kuwatupa baharini, walivua nguo za wafu nakuwafunga durag vichwani mwao, idadi ya durag ilikua inaonyesha idadi ya wafu’

Durag ni kitambaa kinachositiri kichwa ambacho hufungwa ili kuikinga nywele .

Wajackoyah alisema, hayuko tayari kuacha kuvalia durag,alisema anahisi vizuri akiwa amevalia vazi hilo.

‘Napenda huu mtindo ya mavazi, niko na suti lakini nahisi vizuri nikiwa kwa mavazi ya kawaida.

Tume ya IEBC ilimdhinisha Wajackoyah kuwania kiti cha urais pamoja na mgombea mwenza wake Justina Wamae.

Wawili hao  walipata nafasi ya kuonyesha wapiga kura kuhusu ukulima wa bangi kama kitega uchumi. Alisema  kwamba atazindua manifesto yake mnamo Julai 2 mwaka huu.