Martha Karua asherehekea kufikisha miaka 65

Karua ni mama wa watoto wawili na pia ni wakili.

Muhtasari

• Aliyekuwa mgombea mwenza wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Martha Karua anasherehekea siku yake ya kuzalia Alhamis kufikisha umri wa miaka 65.


siku ya kuzaliwa ya Marha Karua
Martha Karua, siku ya kuzaliwa ya Marha Karua
Image: Twitter

Aliyekuwa mgombea mwenza wa chama cha Azimio la Umoja One Kenya Martha Karua alisherehekea siku yake ya kuzalia Alhamis kufikisha umria wa miaka 65.

"Miaka 65 leo na nashukuru Mungu kwa hiyo," Martha alisema.

 Karua alizaliwa mwaka wa 1957 tarehe 22 Septemba na siku hii ameisherehekea kwa njia ya kipekee huku Wakenya wakiungana naye kumtakia heri njema ya kuzaliwa.

Karua ambaye ni mama wa watoto wawili, amekuwa mwanamke wa kuigwa na kielelezo chema si Kenya tu bali hata mataifa mbali mbali ya ughaibuni.

Kiongozi huyowa chama cha Narc aliwahi kuhudumu katika serikali za awali amabpo alijizolea sifa sufufu kutokana na utendakazi wake usio wa mzaha, mpaka wakati mmoja kubatizwa kwa jina la kimajazi Iron Lady.

Karua aliteuliwa kama mgombea mwenza wa kinara wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Katika uchaguzi huo, wapinzani wao wakuu kutoka Kenya Kwanza wakiongozwa na raia wa sasa William Ruto waliwabwaga Azimio na kutangazwa washindi mnamo Agosti 15 na mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.

Iwapo Odinga angeteuliwa kama rais, basi Karua angeingia kwenye vitabu vya historia kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kuhudumu katika ofisi ya naibu rais, si tu chini ya katiba mpya ya mwaka 2010 bali tangia uhuru.

Baada ya jopo la majaji saba kutupilia mbali ombi la Azimio lililotaka kubatilishwa kwa ushindi wa Ruto, Karua alidokeza kwamab kamwe hakukubaliana na uamuzi huo na kusema huenda atatafakari kuelekea katika mahakama ya haki ya ukanda wa Afrika Mashariki ili kudai haki.