Kuna mambo mengi ambayo tunasahau baada ya muda!
Tunapozeeka, tunaanza kugundua kuwa hatuwezi kukumbuka majina ya watu, tulichofanya jana, au kile tulichookota jikoni ... na tunahangaika.
Lakini muda mrefu kabla ya hapo, wengi wetu tayari tumepoteza kitu kingine, karibu bila kutambua: kumbukumbu zetu za kimwili.
Tazama watoto wadogo na utaona kwamba migongo yao ina mkunjo mzuri wa "S" na miondoko yao mithili ya maji.
Bado hawana tabia mbaya ambayo husababisha uchovu na mvutano wa misuli na hatimaye kusababisha mkao mbaya.
Matatizo ya mkao mbaya ni mengi na yanaweza kuumiza, lakini yote yanaweza kuboreshwa kwa mabadiliko machache ya maisha.
Ni vyema kushauriana na daktari wako, mtaalamu wa tiba ya mwili, tabibu au mtaalamu mwingine aliyehitimu kwa ushauri, lakini kwa sasa inaweza kuwa vyema kuzingatia baadhi ya makosa ya kawaida ya mkao yaliyofafanuliwa na mtaalamu wa tiba ya viungo Nick Sinfield.
Wacha tuanze kwa kuketi, lakini ...
Kuketi ukiegemea mbele mara nyingi ni vizuri. Lakini baada ya muda, kukaa namna hii inaweza kuweka shinikizo kwenye misuli na kusababisha maumivu.
Fanya mazoea ya kukaa vizuri. Mara ya kwanza unaweza usijisikie vizuri kwani misuli yako haijazoeshwa kukaa namna sahihi, lakini utaizoea.
2. Usipinde mabega yako
Unapofanya kazi kwenye kompyuta yako kwenye dawati lako, kichwa chako kinaweza kuelekea mbele, ambayo inaweza kuchangia kukuza mgongo wako wa juu, na kwa hivyo mabega kukaza.
Jambo hilo hilo hutokea unapotumia simu yako, ambayo inaweza kusababisha matatizo kama vile ugonjwa wa shingo , ambayo inaweza kusababisha maumivu na ukakamavu kwenye shingo, mgongo na maumivu ya kichwa.
Pamoja na kuzingatia kurekebisha mkao wako, Sinfield inapendekeza eneo la mgongo la juu, shingo kupatiwa mazoezi ya kuimarisha bega, kunyoosha kifua, na mazoezi ya shingo.
Kama vile kichwa chako kinaweza kuelekea mbele unapoketi kazini, shingo yako inaweza kupinda upande mwingine. Ili kuepuka hili...
- Urefushe shingo yako juu kwa upole, ukiingiza kidevu chako ndani.
- Shusha mabega chini
- Legeza misuli ya tumbo la chini ili kudumisha muundo wa asili katika sehemu ya chini ya mgongo
- Rekebisha kiti chako kisiwe chini sana
- Na skrini yako, ili isiwe juu sana.
Sasa, tunainuka, lakini kwanza fanya haya mazoezi rahisi machache ...
Mazoezi kuondoa maumivu ya shingo na shingo iliyokakamaa:
Kunyoosha shingo: Shusha polepole upande wa sikio la kushoto kuelekea bega la kushoto; shikilia pumzi yako na kuachia mara 10 hadi 15, kisha rudia kwa upande mwingine.
Mzunguko wa shingo : Polepole mzunguko wa kidevu kuelekea bega moja; shikilia pumzi ukivuta na kuachia mara 10-15, rudia kwa upande mwingine.
Sasa nyanyuka, lakini...
3. Usisimame kwa mguu mmoja
Ni jambo tunalofanya ili kupumzika tunapolazimika kusimama kwa muda mrefu.
Lakini badala ya kutumia misuli husika ya kukuwezesha wewe kuwa wima, unakuweka shinikizo kupita kiasi upande mmoja wa nyuma yako na nyonga.
Pata mazoea ya kusimama wima kila wakati na uzito wako ukiwa umesambazwa sawasawa kwa miguu yote miwili.
Na wakati wa kufanya hivyo, hakikisha ...
Kuvaa viatu vya visigino virefu na uzito kupita kiasi kuzunguka tumbo kunaweza kusababisha mkao unaojulikana kama "Donald Duck".
Ili kurekebisha hili, fikiria una kamba iliyofungwa kichwani mwako na kuvutwa juu. Wazo ni kuweka mwili wako katika mpangilio kamili, na mkunjo wa asili wa mgongo wako, shingo yako moja kwa moja, na mabega yako sambamba na nyonga yako.
4. Mazoezi ya misuli
Wakati mfupa wa nyonga umepinda huku mgongo wako ukiwa bapa - bila mkunjo wa asili wa chini - mwili wako unainama mbele.
Mkao huu mara nyingi husababishwa na kutokuwepo kwa usawa wa misuli, lakini muda mrefu wa kukaa pia unaweza kuchangia .
Ili kuiboresha, Sinfield inapendekeza mazoezi yenye lengo la kuimarisha misuli ya kiwiliwili, makalio, shingo na nyuma ya mabega.