Kisa cha kushangaza cha wanandoa wenye ulemavu wa macho

Wakati Rashid alikuja kuniomba ndoa nilimuuliza mbona mimi? ukanipenda licha ya hali yangu.

Muhtasari

•Bi Lilian hakuzaliwa akiwa mlemavu wa macho, hali hiyo ilikuja kumpata ukubwani.

• Rashid alipoteza uwezo wa kuona takriban mwaka moja unusu kabla  ya kufunga ndoa na Lilian.

Mwanamume mmoja aliwacha familia yake ikinogoneza baada ya kumuoa mwanamke mwenye ulemavu wa macho.

Mwanamume huyu anayejulikana kama Rashidi ambaye anaishi Arusha, Tanzania,  alifurahia kupindukia  wakati alipokutana  na swahiba wake Liliana ambao wanapendana si kiasi.

Lilian akizungumza na kituo cha Afrimax English alisema hakuwahi kudhania kwamba siku moja atakuwa mke wa mtu, na kwa kuwa binadamu hanyimwi kila kitu, hatimaye alikutana na mpenzi wake Rashid ambaye alimpenda kwa dhati bila kuangalia upungufu wake. 

Kulingana na Lilian, licha ya kufunga ndoa na kuishi pamoja hajawahi kujua sura ya bwanake hata sekunde moja lakini hili halijamzuia kufurahia ndoa na Rashid.

Lilian alisema ''Wakati Rashid alikuja kuniomba ndoa nilimuuliza mbona mimi? ukanipenda licha ya hali yangu'' lakini Rashid alikuwa ameamua kumuoa na wala  hangejirudi nyuma.

Lilian hakuzaliwa akiwa mlemavu wa macho, hali hiyo ilikuja kumpata ukubwani. Alikuwa ameolewa kabla ya kupofuka, lakini baadaye mumewe wa kwanza ambaye alikuwa amepata naye watoto wawili alianza kumtelekeza na hatimaye akamumuacha.

Miaka kadhaa baadae ndipo alipokutana na Rashid.

Ukosefu wa uwezo wa kuona haikubadilisha uamuzi wa Rashidi wa kumuoa Lilian na hivyo akamfanya mpenzi wa maisha yake.

Rashid kwa upande wake alipofuka wakati ambapo alipojikuta jela kwa bila sababu, njama ambayo anasema alipangiwa na ndugu zake ambao hawakumtakia mema. 

Rashid alipoteza uwezo wa kuona takriban mwaka moja unusu kabla  ya kufunga ndoa na Lilian.

Lakini maisha ya wanandoa hawa hayako shwari kwani wanahangaika  kuwalea watoto wao kutokana na hali duni ya maisha.

Wanandoa hao wanahitaji pesa za chakula,  karo, na fedha za mahitaji ya kila siku kwani hakuna hata mmoja wao aliyeajiriwa.