Wafahamu watu maarufu ambao wamekufa na bado wanapata pesa

Forbes limetoa orodha ya watu 13 maarufu waliopata pesa nyingi zaidi duniani baada ya kufariki.

Image: BBC

Jarida la Forbes linalowaangazia watu matajiri zaidi duniani, wiki hii limetoa orodha ya watu 13 maarufu waliopata pesa nyingi zaidi duniani baada ya kufariki.

Miongoni mwa watu hawa ni wanariadha, wasanii, wacheshi na waandishi, ambao hawako tena katika ulimwengu huu na tayari wamekufa, lakini ambao walipata zaidi ya dola milioni 10.

Jarida hili lilianza kuchunguza masuala ya fedha za watu maarufu waliofariki dunia mwaka 2001. Kwa mujibu wa jarida hilo, mapato ya watu maarufu waliofariki mwaka huu yameongezeka kwa asilimia 72 ikilinganishwa na mwaka 2021, ambayo ni rekodi mpya.

Jarida hilo lilitathmini viashiria vya kodi ya mauzo, uhamishaji na mikataba ya leseni ili kuandaa orodha hiyo.

MATANGAZO

Pia ilifanya mahojiano na wataalamu wa fani hiyo.

Hawa ni baadhi ya watu kwenye orodha.

1. JRR Tolkien: (alifariki - 1973)

Image: BBC

Mwandishi maarufu zaidi kwenye orodha hiyo ni JRR Tolkien ambaye aliandika riwaya maarufu kama vile 'Lord of the Rings' na 'The Hobbit'.

 JRR Tolkien, profesa katika Chuo Kikuu cha Oxford, alifariki mnamo 1973, lakini mapato yanaendelea kutiririka kutoka kwa hakimiliki za filamu, katuni na riwaya zingine zenye msingi wa fantasia.

2. Kobe Bryant

Image: BBC

Mwandishi wa Tolkien anafuatwa na nyota wa mpira wa vikapu Kobe Bryant. Hisa zake katika kampuni ya vinywaji vya michezo ya Body Armor zilinunuliwa na Coca-Cola kwa dola milioni 400.

Bryant alifariki huko Santa Monica, California mnamo Januari 2020 baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kuanguka.

3. David Bowie

Image: BBC

 Msanii maarufu David Bowie yuko katika nafasi ya tatu kwa kukusanya dola milioni 250.

4. Michael Jackson

Image: BBC

Pia kwenye orodha hiyo yumo Michael Jackson ambaye aliingiza jumla ya dola milioni 7 baada ya kifo chake.

5. Juan Gabriel

Image: BBC

Hakuna wanawake waliojumuishwa katika orodha hii, huku mwimbaji wa Mexico Juan Gabriel akiwa ndiye nyota pekee kwenye  orodha hiyo kutoka Amerika Kusini.