Fahamu kwanini ni muhimu kula matunda na maganda yake

Matunda na mboga ni vyanzo vikuu vya vitamini, madini, nyuzinyuzi, kemikali nyingi za phytochemicals na antioxidants.

Muhtasari

•Shirika la Afya Ulimwenguni liliripoti kwamba takriban vifo milioni 3.9 kwa mwaka ulimwenguni kote vinahusishwa na watu ambao hawali matunda na mboga za kutosha.

•Baadhi ya watu humenya matunda na mboga kwa sababu wanahofia mabaki ya dawa za kuua wadudu zilitumiwa wakati wa ukuzaji.

Image: BBC

Baadhi ya watu wengi, wanapotayarisha matunda na mboga mboga wana mazoea ya huzimenya. Hata hivyo, mara nyingi sio lazima. Kuna virutubisho muhimu kwenye maganda. Kando na hilo, maganda ya matunda na mboga yanatupwa huchangia mabadiliko ya hali ya hewa.

Matunda na mboga ni vyanzo vikuu vya vitamini, madini, nyuzinyuzi, na kemikali nyingi za phytochemicals (kemikali za mimea) pamoja na antioxidants (vitu vinavyolinda seli).

Kutokula vyakula hivi vyenye virutubishi vya kutosha kunahusishwa na kuongezeka kwa hatari ya magonjwa sugu, pamoja na ugonjwa wa moyo na mishipa na kisukari cha aina ya 2.

Mnamo mwaka wa 2017, Shirika la Afya Ulimwenguni liliripoti kwamba takriban vifo milioni 3.9 kwa mwaka ulimwenguni kote vinahusishwa na watu ambao hawali matunda na mboga za kutosha.

Kula gramu 400 ya matunda na mboga kwa siku, kama ilivyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ni vigumu kwa watu wengi.

Kwa hivyo je, kula matunda na mboga na maganda yake kunaweza kusaidia kwa tatizo hili kwa kuongeza virutubisho muhimu kwenye mlo wa watu?

Bila shaka inaweza kuchangia. Kwa mfano, kiasi kikubwa cha vitamini, kama vile vitamini C na riboflavin na madini kama chuma na zinki hupatikana kwenye maganda ya mboga saba za mizizi: beetroot, haradali ya mwitu, karoti mwitu, viazi vitamu, figili, tangawizi na viazi vyeupe.

Idara ya Kilimo ya Marekani inaonyesha kwamba tufaha ambazo hazijatolewa maganda zina asilimia 15 ya vitamini C zaidi, 267% zaidi ya vitamini K, 20% zaidi ya calcium, 19% zaidi ya potasiamu, na asilimia 85 zaidi ya nyuzinyuzi kulikovile zilizotolewa maganda. Kando na hilo, maganda mengi yana kemikali nyingiza kibaolojia, kama vile flavonoids na polyphenols, ambazo ni muhimu kwa afya.

Sababu nyingine ya kutotupa maganda ya matunda na mboga ni athari ya maganda hayo kwa mazingira. Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, chakula kisicholiwa, ikiwa ni pamoja na maganda, hutoa kati ya 8% na 10% ya uzalishaji wa gesi chafu duniani. Chakula kinachooza kwenye dampo hutoa methane, gesi chafu yenye nguvu zaidi.

New Zealand, nchi ambayo ina watu milioni 5.1 pekee, inaripoti upotevu wa tani 13,658 za maganda ya mboga na tani 986 za maganda ya matunda kila mwaka.

Kwa kuzingatia maudhui ya virutubishi kwenye maganda, na mchango wa maganda hayo katika upotevu wa chakula, kwa nini watu humenya matunda na mboga?

Baadhi matunga na mboga lazima zitolewe maganda, kwa vile sehemu za nje haziliwi, hazina ladha nzuri, ni ngumu kusafishwa, au kusababisha uharibifu, kama vile ndizi, chungwa, tikitimaji, nanasi, embe, parachichi na kitunguu saumu.

Pia, kuwasafisha kunaweza kuwa sehemu ya lazima ya mapishi, kama vile wakati wa kutengeneza viazi zilizosokotwa. Lakini maganda mengine kama za viazi, beetroot, karoti, kiwi na tango, yanaweza kuliwa, ingawa watu huyamenya.

Mabaki ya dawa

Baadhi ya watu humenya matunda na mboga kwa sababu wanahofia mabaki ya dawa za kuua wadudu zilitumiwa wakati wa ukuzaji.

Mabaki ya dawa husali kwa kiasi kidogo, ingawa hii inatofautiana na spishi za mimea. Hata hivyo, mengi ya mabaki haya yanaweza kuondolewa kwa kuosha.

Kwa kweli, Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani inapendekeza kwamba watu wanawe vizuri katika maji baridi na kusugua kwa brashi ngumu ili kuondoa dawa za kuulia wadudu, uchafu, na kemikali.

Mbinu za mapishi, kama vile kuchemsha na kutumia mvuke, zinaweza pia kupunguza mabaki ya dawa.

Lakini si mabaki yote ya dawa ya wadudu huondolewa kwa kuosha na kupika. Ndio sababu watu wanaohofia uwezekano wao wa kuathiriwa na dawa za kuulia wadudu wanaamua kumenya matunda na mboga.

Katika baadhi ya nchi kuna orodha za kiasi cha dawa za kuua wadudu kwenye matunda na mboga, kama vile ile inayotolewa na Pesticide Action Network for the United Kingdom. Hii inaweza kukusaidia kuamua ni matunda na mboga gani ya kumenya.