Utafiti: Binadamu na Sokwe wanaelewa lugha moja

Wanasayansi walitumia majaribio ya kurudiarudia video

Muhtasari

Timu hii ya watafiti imetumia miaka mingi kuwachunguza sokwe-mwitu

Sokwe mwitu
Sokwe mwitu
Image: BBC

Binadamu wanaelewa "ishara" ambazo sokwe mwitu na bonobo hutumia kuwasiliana wao kwa wao. Hilo ndilo hitimisho la utafiti wa video ambapo watu waliojitolea walitafsiri ishara za viumbe hao pamoja na nyani. Ilifanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha St Andrews.

Utafiti huo unaonyesha kwamba kizazi cha babu wa mwisho aliyekuwa na uhusiano wa pamoja na sokwe alitumia ishara zinazofanana, na kwamba ishara hizi zilikuwa "mahali pa kuanzia" kwa lugha yetu.

Matokeo yamechapishwa katika jarida la kisayansi la PLOS Biology. Mtafiti mkuu, Dk Kirsty Graham kutoka Chuo Kikuu cha St Andrews alieleza: "Tunajua kwamba aina hii ya wanyama sokwe, nyani wote wakubwa na bonobos - wana mwingiliano wa takriban 95% ya ishara wanazotumia kuwasiliana.

"Kwa hivyo tayari tulikuwa na udadisi na hisia kwamba huu ulikuwa uwezo wa ishara wa pamoja ambao unaweza kuwa ulikuwepo kwa mababu zetu wa mwisho. Lakini tuna uhakika kabisa kwamba mababu zetu walitumia ishara, na kwamba ishara hizo zilijumuishwa katika lugha. ."

Utafiti huu ulikuwa sehemu ya dhamira inayoendelea ya kisayansi kuelewa simulizi hii ya asili ya lugha kwa kusoma kwa makini mawasiliano kupitia nyani na sokwa wenye ukaribu wa kibailojoia na kihistoria na binadamu.

Timu hii ya watafiti imetumia miaka mingi kuwachunguza sokwe-mwitu. Hapo awali waligundua kwamba viumbe hao wakubwa hutumia ishara zaidi ya 80, kila mmoja akiwasilisha ujumbe kwa mwenzake ndani ya kikundi chao.

Jumbe kama vile "kumfundisha" huwasilishwa kwa mwendo mrefu wa kukwaruza; kutikisa mdomo kinamaanisha "nipe chakula hicho" na kurarua vipande vya jani kwa kutumia meno ni ishara ya kutaniana.

Wanasayansi walitumia majaribio ya kurudiarudia video, kwa sababu mbinu hiyo imetumika kwa kawaida kujaribu ufahamu wa lugha katika viumbe wasiokuwa binadamu.

Katika utafiti huu, waligeuza mbinu hii na kutathmini uwezo wa wanadamu kuelewa ishara za jamaa zao wa karibu wa nyani. Lugha ya sokwe mwitu imetafsiriwa.

Watu waliojitolea walitazama video za sokwe na bonobo wakionyesha ishara, kisha wakachaguliwa kutoka orodha nyingi za chaguo za tafsiri.

Washiriki walifanya vizuri zaidi kuliko ilivyotarajiwa, wakifasiri kwa usahihi maana ya ishara za sokwe na bonobo kwa zaidi ya asilimia 50% ya wakati huo.

"Tulishangazwa sana na matokeo," alisema Dk Catherine Hobaiter kutoka Chuo Kikuu cha St Andrews. "Inavutia kuona mageuzi ya mtazamo wa mawasiliano na inakera sana kwa mwanasayansi ambaye alitumia miaka mingi kujifunza jinsi ya kuifanya," alitania.

Ishara ambazo watu wanaweza kuelewa kwa asili zinaweza kuwa sehemu ya kile Dk Graham alichoelezea kama "msamiati wa mageuzi ya kale, ya pamoja ya ishara katika spishi zote kubwa za nyani pamoja na sisi".