Ni nini husababisha mdomo kunuka? Mtaalamu wa afya ya meno anajibu

"Njia bora zaidi ya kupiga mswaki ni kwa kupiga mswaki kwa njia nyepesi na sio kupiga mswaki kwa nguvu" mtaalamu alihoji.

Muhtasari

• Halitosis, ambayo ni hali ya kunuka kwa mdomo husababishwa na vitu vingi ambavyo ni kutoka nje na ndani ya mdomo wako.

Image: Maktaba

Wataalamu wa afya ya meno wamesema kuzuia na kutibu harufu ya kinywa kunaweza kupita zaidi ya kupiga mswaki mara mbili kila siku, wakibainisha kuwa baadhi ya magonjwa ya masikio na pua yanaweza kusababisha hali hiyo inayojulikana kama halitosis.

Halitosis ni tatizo la afya ya kinywa ambapo dalili kuu ni harufu mbaya ya kinywa.

Wataalamu hao pia wameeleza kuwa baadhi ya vyakula vinaweza kusababisha halitosis na kuwataka Watu kuwa makini na kile wanachokula.

Huku wakibainisha kuwa mbinu mbovu za kupiga mswaki pamoja na kupuuza ulimi zinaweza pia kusababisha harufu mbaya mdomoni, wataalam hao waliwashauri Watu kukumbatia tabia ya kumtembelea daktari wa meno mara moja kila baada ya miezi sita kwa ajili ya kutathmini afya ya meno.

Walisisitiza kuwa kuna kikomo kwa kile ambacho miswaki inaweza kufanya, wakibaini kuwa kutathmini afya ya meno ni muhimu.

Halitosis, walisema, inaweza kuwa ya aibu kwa mgonjwa na inaweza kusababisha mtu kujishusha thamani.

"Sababu ya halitosis sio moja kwa moja. Harufu ya kinywa inaweza kutoka nje ya kinywa na ndani ya kinywa. Ikiwa iko ndani ya kinywa, inaweza kuwa kutoka kwa mkusanyiko wa uchafu na bakteria ya plaque kwenye kinywa. Kisha nje ya mdomo, inaweza kuwa kutoka kwa chakula ambacho mtu anakula, kama vile kitunguu saumu, na vitunguu, basi kwa watu wengine ambao wana vidonda vya tumbo, inaweza kusababisha harufu mbaya mdomoni wakati mwingine.”

"Halafu ikiwa mtu ana ugonjwa wa pua au sikio, unaweza kusababisha harufu mbaya mdomoni, Jambo lingine ni kwamba watu wasipopiga mswaki vizuri, wanaweza kuwa na halitosis. Jambo lingine ni kwamba wakati wa mfungo watu huwa na harufu mbaya ya kinywa pia” Daktari alihoji.

Pia harufu ya kinywa chako ikitoka kwa ugonjwa kama vile kidonda au kisukari, kuyatibu ndiyo yanaondoa harufu mbaya mdomoni kwani hata ukipiga mswaki kiasi gani na kutunza mdomo wako, hutaondoa harufu – suluhu ni kutimu magonjwa haya tu!

Njia bora zaidi ya kupiga mswaki ni kwa kupiga mswaki kwa njia nyepesi na sio kupiga mswaki kwa nguvu. Wengi wetu tuna mawazo haya kwamba kadri tunavyopiga mswaki kwa ugumu ndivyo inavyokuwa bora kwa meno yetu na ni rahisi kwetu kuondoa harufu ya kinywa. Kwa hivyo, utaona watu wananunua miswaki hii ngumu kwa sababu hiyo lakini sivyo, mtaalamu wa afya ya meno alishauri.