Je, unashangaa ni kwa nini unapoteza kilo za mwili kwa kasi? Hizi hapa ni baadhi ya sababu

Ukiwa unapunguza uzito bila kukusudia au bila juhudi yoyote kunaweza kuwa na matatizo zaidi ambayo yanapswa kuchunguzwa.

Muhtasari

• Kupunguza uzito bila kukusudia kunaweza kusababisha na matatizo ya msongo wa mawazo na pia sababau za kiafya.

• Baadhi ya sababu hizi ni matukio ya ghafla kama vile talaka, kupoteza kazi, au kifo cha mpendwa. Inaweza pia kusababishwa na utapiamlo au hali ya kiafya.

Mtu aliyepunguza uzito wa kilo.
Mtu aliyepunguza uzito wa kilo.
Image: BBC NEWS

Unapokuwa kwenye safari ya kupunguza uzito, kupunguza kila kilo lazima kusherehekewe kwani unakuja kwa juhudi kubwa.

Lakini ikiwa unapunguza uzito bila kukusudia au bila juhudi yoyote kunaweza kua na matatizo zaidi ambayo yanapswa kuchunguzwa.

Kupunguza uzito bila kukusudia kunaweza kusababisha na matatizo ya msongo wa mawazo na pia sababau za kiafya.

Watu wengi wanaambaatanisha kupungua kwa uzito kwa sababu za kiafya peke yake lakini hii si kweli kwa kuwa kupunguza kwa uzani kuna sababu nyingi.

Baadhi ya sababu hizi ni matukio ya ghafla kama vile talaka, kupoteza kazi, au kifo cha mpendwa. Inaweza pia kusababishwa na utapiamlo au hali ya kiafya.

Kwa wakati huu mgumu wa kiuchumi mojawapo ya sababu kuu ni hali za afya ya akili, kama vile unyogovu, wasiwasi na matatizo ya kula.

Licha ya  matatizo ya msongo wa mawazo pia kuna matatzio ya kiafya kama vile matatizo ya usagaji wa chakula mwilini, ugonjwa wa celiac.

Pia hali zingine za kiafya, kama vile ugonjwa kisukari aina ya pili, ugonjwa wa moyo au pia kifua kikuu.

Wakati mwingine kupoteza uzito kunaweza kusababishwa na saratani.

Ni muhimu kuchunguzwa ikiwa unapunguza uzito bila mazoezo ama bila kutaka.