logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chakula asili kinachoweza kuongeza ari ya ngono

Kwa kuvitumia unaweza kutosheleza hamu ya mpenzi wako katika tendo la ndoa

image
na

Yanayojiri11 July 2023 - 07:09

Muhtasari


•Hivi ni baadhi tu ya vyakula japokuwa kuna vingine vinavyoweza kusaidia na kuboresha hamu ya kushiriki tendo la ndoa kama vile; mihogo, njugu karanga, mbegu za malenge na chokoleti.

Mwanaume afariki kwa kudungwa sindano ya kuongeza uume.

Inadaiwa kuwa ndoa nyingi na mahusiano huweza kusambarika kutokana na sababu nyingi; sababu ya kutoshelezana katika mapenzi ikiwepo.

Kutoshelezana katika mapenzi huyapa mahusiano msingi thabiti na kuaminiana baina ya wapenzi, na kinyume chake iwapo jambo hili halitafanyika basi huchangia kwa kiwango kikubwa kusalitiniana katika mapenzi.

Kutoaminiana katika mahusiano huchangia mambo mengi baina ya wapenzi ambayo mengine yanaweza kuleta maafa katika afya ya binadamu, hasa wanapotumia vitembe vya kuongeza nguvu za kiume.

Wengine hujipata katika hali ya ugonjwa wa moyo na ule wa akili, iwapo anahisi kuwa mpenziwe anamdharau au hajamtosheleza alivyotamani katika tendo la ndoa kwa muda ambao mwanadada anahisi kuwa ameridhika.

Kumekuwa na visa vya watu kufariki wakijaribu kuongeza nguvu za kiume. Baadhi yao huwa wanameza vigra au kufanyiwa upasuaji wa nyeti zao ndipo ziweze kuongezwa.

Ili kuongeza hamu ya kuweza kushiriki  mapenzi, daktari wa masuala ya ngono anashauri wapenzi waweze kutumia chakula asili na wala si vitembe vya kemikali au kujidunga sindano ndipo kuongeza nguvu hizo.

Kutumia vyakula kama ninavyoorodhesha, vitakupa motisha na hamu ya kuweza kushiriki mapenzi hadi upate uaminimu na utoshelezaji unaokadiriwa na mpenzi wako.

Avokado au parachichi; Tunda hili huwa na vitamini B6 ambayo huongeza nguvu za mwili wote kwa ujumla.

Tikitimaji; Tikitimaji huwezesha mishipa ya damu kutulia na kusafirisha damu katika mishipa hiyo bila pingamizi lolote. Tunda hili huwezesha damu kusambaa hadi katika sehemu nyeti na hivyo kumpa mtu hamu ya kufanya mapenzi.

Ndizi mbivu; Ndizi zilizoiva zinaaminiwa kuwa chanzo cha potasiamu ambayo ni madini muhimu kwa misuli. Madini hayo husaidia misuli kutulia na kuwa tayari kwa tendo la ndoa na hivyo kumpa mtu hamu kubwa kushiriki katika tendo la ndoa.

Kitunguu saumu; katika mapishi, andaa vyakula kwa kutumia kitunguu saumu. Kiungo hiki huwa na alisini ambayo ni muhimu kwa usafirishaji wa damu katika viungo vingine vya mwili. Damu ya kutosha ifikapo katika sehemu nyeti humpa mtu hamu ya kushiriki ngono.

Spinach; Hii si mboga tu, bali pia ni kiungo muhimu ambacho hutumiwa kuboresha usafirishaji wa damu kwenye viungo vya mwili. Spinach huwa na magneziamu ambayo husaidia kupunga kujikunja kwa mishipa ya damu ili kuwezesha damu kusambaa kwa urahisi na kumpa mtu hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Hivi ni baadhi tu ya vyakula japokuwa kuna vingine vinavyoweza kusaidia na kuboresha hamu ya kushiriki tendo la ndoa kama vile; mihogo, njugu karanga, mbegu za malenge na chokoleti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved