logo

NOW ON AIR

Listen in Live

World Coin: Je ungeruhusu kamera kuchanganua mboni ya jicho lako ili kupata pesa?

Mwanzilishi wa fedha ya kidijitali ya World Coin - sarafu mpya ya kidijitali anataka watu kuanza kutumia sarafu hiyo na mtandao wake.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri01 August 2023 - 03:52

Muhtasari


•World Coin ni miongoni mwa mradi mpya wa fedha za kidijitali . `Unachopaswa kufanya ni kuangalia katika kamera hii kwa jina Orb.

•Na kuhusu mboni yako ya jicho iliochanganuliwa , World coin inasema kwamba maelezo yote hufutwa mara moja.

Hivi ndivyo kamera hizi kubwa zinavyofanya . Ni miongoni mwa mradi mpya wa fedha za kidijitali . `Unachopaswa kufanya ni kuangalia katika kamera hii kwa jina Orb.

Na baadaye unapatiwa fedha za kidijitali …. Kwa kweli utachanganyikiwa.

Mwanzilishi wa fedha ya kidijitali ya World Coin - sarafu mpya ya kidijitali anataka watu kuanza kutumia sarafu hiyo na mtandao wake.

Lakini wanataka uthibitishe kwamba wewe ni binadamu wa kawaida kwa kuchanganua mboni ya jicho lako.

`Nilienda katika kituo chao kimoja. huyu ni mimi nikishikilia Orb. Ilinichukua takriban sekunde kumi kuangalia kamera hiyo ya kidijitali, halafu ikapiga kelele ya ishara kwamba inafanya kazi.

Mboni ya jicho langu ilipatiwa nambari tofauti na kuwekwa katika rekodi za kampuni hiyo ambazo inasema ina takriban rekodi za binadamu milioni mbili waliothibitishwa.

Ilipopiga kelele kwa mara nyengine ilithibitisha kwamba maelezo yangu yote yameongezwa katika rekodi hiyo.

Hii ikimaanisha kwamba sasa naweza kutumia sarafu ya kidijitali ya World coin katika siku zijjazo . `Pia nilipatiwa takriban dola $51 ambazo tutawapatia Watoto kutoka jjamii masikini( Shirika la hisani la BBC).

Na kuhusu mboni yako ya jicho iliochanganuliwa , World coin inasema kwamba maelezo yote hufutwa mara moja.

Lengo kuu ni kujenga utambulisho ulio salama unaojulikana kama KItambulisho cha dunia au World ID.

Lengo letu ni moja : Kujenga mtandao wa kifedha duniani uliothibitishwa, Mwanzilishi mwenza wa mtandao huo Atlman alinukuliwa akisema katika mtandao wa twitter.

Hatahivyo wataalam wa kibinafsi wanasema kwamba wan wasiwasi kwamba maelezo hayo huenda yakaishia katika mikono mibaya.

Na wengine wana wasiwasi kwamba mpango wote huo unaogofya.

Wanaopata fedha hizo wanaweza kuzihamisha katika ubadilishanaji wa fedha za kidijitali kama vile Binance na kuzitumia kununu sarafu nynegine za kidijitali ambazo baadaye zinaweza kuuzwa na kujipatia fedha za bure.

Siku ya Ijumaa mamia ya Wakenya walitembea angalau maduka 13 ya Quick mart ambapo kamera hizo za kidijitali zimewekwa nchini Kenya.

Kulingana na uchunguzi wa waandishi wa gazeti la Nation waliotembelea kituo kimoja cha duka hilo la jumla cha Thome , vijjana wadogo kati ya umri wa miaka 20 na 30 walikuwa wamekusanyika katika maeneo hayo tayari kuhudumiwa.

‘’Unaposikia mtu anatoa fedha za bure ili kujiunga na mtandao wao , huna cha kupoteza , mwanzo sijali kwasababu wanacotaka ni kuchanganua mboni ya jicho langu ‘’, alisema mmoja ya vijana hao akizungumza na gazeti la Daily nation nchini Kenya.

Lakini je washiriki wana cha kupoteza kwa kweli?

Kulingana na gazeti la Daily Nation, World coin na waanzilishi wake hawana habari kuhusu hilo.

‘’Safari hii itakuwa na changamoto chungu nzima na matokeo yake hayajulikani’’, ilisema taarifa ya ufunguzi ya Altman na `blania katika tovuti yao.

Afisi ya kamishna anayelinda data aliwaonya Wakenya dhidi ya kupeana rekodi za maelezo yao ya kibinafsi kabla ya kupokea maelezo kuhusu jinsi data zao zitakavyotumika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved