Idadi ya waliofariki Morocco kwa zilizala yazidi 2000, je, ni nini husababisha zilizala?

Kuna tetemeko la ardhi ambalo hutoa nishati katika mawimbi ambayo husafiri kupitia ukanda wa dunia na kusababisha kutetemeka tunayohisi.

Muhtasari

• Kulingana na wasomi wakuu wa maswala yanayohusiana na maswala ya tetemeko la ardhi ni kuwa hatuwezi kuzuia tetemeko la ardhi.

• Mtetemeko wa ardhi hutokea popote duniani ,wakati wowote wa mwaka kwa hakika haiwezekani kuamua ni wapi na ni lini.

Image: BBC

 Wengi hujiuliza tetemeko la ardi ni nini? Hili hapa jibu lake,

Tetemeko la ardhi ni jambo asili na ambalo hutajwa kwa uharibifu mwingi wa mali kwa kuwa hutokea kwa kasi sana bila kutarajiwa.

Tetemeko hili hutajwa kuletwa na milipuko ya volcano ambayo husababishwa na milipuko ya chini ya ardhi.

Kulingana na historia ya dunia kuwa sahani za tectonic daima zinasonga polepole lakini hukwama kwenye kingo zao kwa sababu ya msuguano.

Kuna tetemeko la ardhi ambalo hutoa nishati katika mawimbi ambayo husafiri kupitia ukanda wa dunia na kusababisha kutetemeka  tunayohisi.

Fahamu kuwa tetemeko kuu duniani 7.0-7.9 na inaweza kusababisha uharibifu mkubwa duniani

Kulingana na wasomi wakuu wa maswala yanayohusiana na maswala ya tetemeko la ardhi ni kuwa hatuwezi kuzuia tetemeko la ardhi bali tunaweza kuzuia au kupunguza madhara yake kwa kutoa elimu kuhusu usalama wa tetemeko la ardhi.

Mtetemeko wa ardhi hutokea popote duniani ,wakati wowote wa mwaka kwa hakika haiwezekani kuamua ni wapi na ni lini na jinsi tetemeko la ardhi litakuwa na nguvu.

Mara mingi tetemeko la ardhi linapotoke husababisha majumba mengi kuanguka na pia milipuko mikubwa husababisha sehemu mbalimbali kutenganishwa huku watu wengi huachwa bila nyumba na pia magojwa mbalimbali hutokea wakiwemo watu wengi kuwa walemavu na mayatima.

Je? kunapotokea tetemeko la ardhi unapaswa kufanya nini. Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia katika tukio la tetemeko la ardhi ,lakini suala la msingi ni linalosisitizwa na wataalamu ni kutulia .

 Wakati wa tetemeko la ardhi hupaswi kukimbia kwani ni hatari kwa usalama wako mbali unafaa kutulia ulipo na kutafuta njia za kutoka ikiwa kunazidi kuwa na hatari unapaswa kuwajuza maafisa wa vikosi vya mikasa ya mlipuko wa ardhi.