Zifahamu Faida za mbegu za papai kwa mwili wa mwanadamu

Mbegu hizi zina virutubisho ambavyo ni muhimu vya kupambana na aina mbali mbali za magonjwa kwa mwilini.

Muhtasari

•Watafiti wa maswala ya kiafya, wamefanya utafiti na kubaini faida muhimu za mbegu za tunda hili la Papai, ambazo watu hutupa baada ya kula tunda lenyewe.

 

Je wajua vyema umuhimu papai? Papai ni tunda linalotambulika zaidi lenye afya. Tunda hili lina madini ya 'antioxidants' ambayo kulingana na utafiti wa wanasayansi,husaidia kupunguza kukinga maradhi mengi mwilini .

Tunda hili pia lina virutubisho ambavyo ni muhimu sana kwa mwili kama vile; Kalori,Protini,Vitamini C, Vitamini A, Vitamini B9, Potasiamu, Kalsiamu Wanga na Magnesiamu.

Watafiti wa maswala ya kiafya, wamefanya utafiti na kubaini faida muhimu za mbegu za tunda hili la Papai, ambazo watu hutupa baada ya kula tunda lenyewe.

Zifuatazo nifaida za mbegu za tunda la papai:

1.Hupunguza kuvimba.

Mbegu za papai zimedhibitishwa kuwa na ufanisi katika kupunguza uvimbe. Zina vitamini C na misombo kama alkaloids, flavonoids, n polyphenols.Misombo hii yote inaonyesha mali ya kupinga uchochezi( anti-inflamatory properties)Kwa hivyo ni muhimu katika kuzuia na kupiunguza uvimbe katika katika magonjwa kama, gout, artheritis na kathalika.

2.Husaidia katika kupunguza uzito wa mwili.

Mbegu za papai zina nyuzinyuzi nyingi mbazo huweka husagaji wa chakula kwa mwili wa binadamiu kwenye laini, na husaidia kuondoa sumu kwa mwili. Pia husaidia katika kudhibiti kimetaboliki yetu na kuzuia mwili wetu kunyonya mafuta ambayo huzuia fetma.

3.Hupunguza maumivu ya wakati wa hedhi.

Mbegu za papai zina crarotene na dutu ambayo ni muhimu kwa kusaidia mwili kughibiti utengenezaji wa homoni inayojulikana kama estrogen.Ingawa mbegu hizi zinaweza kusaidia kupata hedhi na pia kuongeza mzunguko wake, zinasaidia pia kwa kiwango fulani katika kudhibiti maumivu ya wakatoi ya hedhi.

4.Gesi na Ukosefu wa Chakula:

Papai hupunguza asidi tumboni, ikiwa mtu ana kiungulia na maumivu ya tumbo . Papai pia ni tiba ya kusaga chakula tumboni.

5.Afya ya Mifupa:

Mbegu za Papai huongeza ufyonzaji wa kalsiamu kutoka kwenye mifupa, hupunguza utolewaji wa kalsiamu na figo, na huwa na protini zinazolinda mifupa, ambazo zote kwa pamoja husababisha mifupa yenye afya.

6.Hutibu magonjwa ya dengue:

Dengue ni virusi vinavyoenezwa na mbu, ambavyo huathiri chembe za damu kwenye damu yako na huanza kuaribu chembe chembe za afya.Mbegu hizi zimeonyesha kuboresha hezabu za platelet katika masomo ya wanyama. Hivyo zitasaidia sana katika uponaji wa dengi.

Tahadhari:

Watafiti na wanasayansi wanashauri kuwa, japo mbegu hizo zina umuhimu wa asilimia kubwa, zitumike kwa kiwango cha wastan kwani utumiaji wa kupita kiasi una maovu madogo madogo kama kuendesha, kupunguza uwezo wa kuzalisha kwa wanaume, na vile vile haziruhusiwi kwa wanawake wanaonyonyesha.