Najutia kumwambukiza mpenzi wangu ukimwi-Mwanamume asimulia jinsi alivyovunja uhusiano wake

Nani atatuonyesha mwelekeo unaofaa,kuhusu uhusiano wa kimapenzi na ndoa zetu?

Muhtasari
  • Tumeona na kushuhudia wengi wakiuawa na kuuwana kwa ajili ya mapenzi na maisha ya mtu asiye na hatia kukatizwa.
Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.
Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.
Image: Maktaba

Wakati huu na nyakati za sasa uhusiano wa kimapenzi sio jambo la maana au kitilia maanani kwa wengi kwani wamelichukulia kwa dharau.

Wengi ambao wanaingia kwenye uhusiano na wenzi wao, huwa hawamalizi miaka kama akina babu zetu kwani wengi hudanganya katika uhusiano na kusababisha kutengana na madhara kubwa.

Tumeona na kushuhudia wengi wakiuawa na kuuwana kwa ajili ya mapenzi na maisha ya mtu asiye na hatia kukatizwa.

Swali kuu ambalo huwa najiuliza kila mara na kila siku, kwa nini watu wasichukulia uhusiano kwa umakini na kuheshimu uhusiano huo kama akina babu zetu?

Ni swali ambalo halina jibu kwani kizazi cha sasa wanatambua ngono ndio kitu ya maana katika uhusiano.

Ndio ni wengi wameumizwa miyo na kuapa kwamba hawatawahi kujihusisha na uhusiano tena.

Ndio maana idadi ya kuwa 'single mothers' imeongeza mara dufu duniani, kwani wengi walitaka kutimiza tu mahitaji yao ya ngono na kumuacha mwanamke huyo na ujauzito, na kumlea mwanawe.

Sio tu kizazi hiki pekee ambacho hakina heshima na uhusiano, kwani tumewaona akina baba zetu wakituonyesha mkondo huo wa kutohehsimu uhusiano na ndoa, kwa sababu wamekuwa na mipango ya kando, ambao wana umri mchanga san.

Nani atatuonyesha mwelekeo unaofaa,kuhusu uhusiano wa kimapenzi na ndoa zetu?

Mwanamume mmoja aliwaacha wanamitandao na gumzo vinywani baada ya kusimulia jinsi alivyo mwambukiza mpenzi wake virusi vya ukimwi.

"Najuta kumwambukiza mpenzi wangu virusi vya ukimwi,mpenzi wangu hajawahi nicheat na mtu mwingine kwani alikuwan ameniamini kuwa pia siwezi mcheat alikuwa busy sana na kazi zake lakini nashukuru alikuwa anatenga muda niweze kukaa na yeye,uhusiano wetu tulikuwa tunataka kuupeleka upande mwingine wa ndoa, lakini ni kama nilikuwa nimerogwa na kuona wanawake, siwezi danganya nimemcheat mpenzi wangu na wanawake wengi,siwezi hata hesabu

Juzi alipata scholarship ya kuenda majuu na mimi nikakubali kwani nilijua mahitaji mengine nitatimiziwa,lakini aliniambia kuwa anataka twende tukapimwe virusi vya ukimwi,nilimwambia aende pekeyake kwani niko sawa

Alipoenda alipatikana na virusi vya ukimwi,alinipigian simu na kutoka wakati huo wamenipa block,najua ni mimi nilimuambukiza kwaninilicheza vibaya,"Alisimulia.