Niliambukizwa virusi vya ukimwi na bosi wangu-Mwanadada amwaya mtama kwa uchungu

Kulingana na Janet alipokuwa akitafuta kazi baada ya kuhitimu alipatana na bosi wake kwenye kazi yake mpya na kisha wakakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Muhtasari
  • Ni mambo ambayo vipusa na wanaume wanafanya wakati huu wa sasa na mwishowe kujuta na kujipata pabaya.
Mwanamke mwenye huzuni
Mwanamke mwenye huzuni
Image: HISANI

Je ni jambo lipi ambalo umewahi kufanya maishani mwako na kujuta baada ya miaka kadhaa au jambo ambalo lilikuletea madhara makubwa maishani mwako?

Ni mambo ambayo vipusa na wanaume wanafanya wakati huu wa sasa na mwishowe kujuta na kujipata pabaya.

Ndio tumeona katika taarifa na habari kila siku jinsi vijana nchini wanatafuta kazi licha ya kuwa na ukosefu wa kazi.

Kila mtu anapohitimu chuo kikuu huwa na matumaini ya upata kazi na kuendelea maisha yake kama kawaida, kwani huwezi tegemea wazazi kwa kila jambo.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii mwanadada mmoja alisimulia jambo ambalo amejuta kwa kufanya.

Kulingana na Janet alipokuwa akitafuta kazi baada ya kuhitimu alipatana na bosi wake kwenye kazi yake mpya na kisha wakakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Bila ya kujua bosi wake alikuwa na virusi vya ukimwi aliweza kumpa kila kitu licha yake kuwa na mpenzi.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilipata kazi mjini Nakuru bosi wangu alikuwa mtu mwema, bila kujua ama wacha niseme kwa ajili ya tamaa yangu kutaka kukaa katika kazi hiyo, niliweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi huyo, uhusiano wetu ulienda kutoka kiwango kimoja hadi kingine

Alikataa kabisa twende VCT kwa madai kwamba napaswa kumwamini,ndio sijui ni ujinga ama nilimwamini kabisa,wakati wa hayo yote nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tumetoana mbali naye, wakati mmoja nilienda kupimwa virusi vya ukimwi na nikapatikana nazo, nina uhakika kuwa bosi wangu ndiye aliyeniambukiza, sijui ni mwambie mpenzi wangu nini au niachane naye kwani sitaki kumwambukiza

Najuta sana kujihusisha kwa jambo kama hilo maishani mwangu."

Kwa wasichana wadogo wanaomaliza shule haya basi maisha ni polepole wacheni kutaka kupanda mti kutoka juu kwani utajipata pabaya na kisha kuwaletea wazazi mzigo mwingine.