Krisimasi ni nini na ni kwanini Wakristo wanaisherehekea?

Siku ya Krismasi ni fursa ya kutulia na kushukuru kwa upendo, tumaini na furaha inayopatikana katika Yesu

Muhtasari
  • Ni nani aliyefanya uamuzi wa kuadhinishwa Krismasi tarehe 25 Disemba?
  • Baadhi ya nyaraka zinasema alikuwa papa; lakini wengine wanasema sio kweli.

Kila mwaka, duniani kote, waumini wa Kikristo husherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo Siku ya Krismasi, tarehe 25 Disemba. Ni siku - na msimu - ulioyojaa nyimbo za Krismasi, kupamba miti, kupeana zawadi na karamu.

Na, kati ya sherehe zote, unaweza kujiuliza: Ni nini maana halisi ya Krismasi? Au, Kwa nini kuna utamaduni wa Krismasi? Je, una uhusiano gani na Yesu?

Krismasi husherehekewa tarehe Disemba 25, lakini haikuwa hivyo kila mara.

Disemba 25 si tarehe inayotajwa katika Biblia kuwa siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Biblia kwa kweli haisemi siku au wakati wa mwaka ambapo Mariamu (Bikra Maria) ilisemekana kuwa alimzaa katika mji wa Bethlehemu.

Ni nani aliyefanya uamuzi wa kuadhinishwa Krismasi tarehe 25 Disemba?

Baadhi ya nyaraka zinasema alikuwa papa; lakini wengine wanasema sio kweli.

Hatahivyo nyaraka na maelezo mengi yanaonyesha kuwa , siku ya kuzaliwa kwa Yesu ilifikiriwa kwa mara ya kwanza - karibu 200 AD na ilianza kwa kuadhimishwa tarehe 6 Januari.

Kufikia katikati ya karne ya 4, sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ilikuwa Desemba 25.

Lakini Wakristo wa dhehebu la Orthodox husheherekea Krismasi Januari 7, badala ya Disemba 25, iliyozoeleka na wengi. Unaweza kuiita Krismasi ya Orthodox.

Wakristo wa dhehebu la Orthodox hufuata kalenda tofauti na kalenda ya Gregorian ambayo kawaida hutumika katika nchi za Magharibi.

Wanasherehekea Krismasi tarehe 7 Januari, na sherehe zikianza rasmi usiku wa manane katika mkesha wao wa Krismasi.

Julius Caesar alianzisha kalenda katika 46BC kulingana na ushauri wa mwana-astronomia wa Misri Sosigene, ambaye alikuwa amehesabu mwaka wa mwezi

Ni kwanini Wakristo wanasherehekea Krisimasi?

Kwa Wakristo Krismasi inahusu kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu – Yesu Kristo. Inahusu jinsi alivyokuja duniani kuwapa upendo, tumaini na furaha. Ujumbe huo haubadiliki mwaka hadi mwaka.

Biblia inasema nini kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo?

Kulingana kitabu cha Biblia kinachotumika kama mwongozo wa Ukristo, malaika Gabrieli alimtokea kwa mara ya kwanza mwanamke kijana anayeitwa Mariamu. Alimwambia kwamba amechaguliwa kuwa mama ya Yesu - yaani, atamzaa Mwana wa Mungu.

“Usiogope, Mariamu; umepata kibali kwa Mungu. Utachukua mimba na utamzaa mtoto mwanamume, nawe utamwita Yesu,” malaika akasema (Injili ya Luka 1:30-31), toleo la Biblia ya Habari Njema, kisha mariamu akapata mimba kwa uwezo wa Roho mtakatifu na kumzaa Yesu kristo

Sikukuu ya Krisimasi ina maana gani kwa Wakristo?

kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni zaidi ya sikukuu ya Kikristo.

Ni zaidi ya tukio la kupamba nyumba na kuburudika kwa vyakula na vinywaji , kupeana zawadi na kufurahi na wapendwa.

Krismasi inachukuliwa kama kumbukumbu ya upendo ambao Mwenyezi Mungu aliupenda ulimwengu na kumtoa mwanaye wa pekee ili aukomboe ulimwengu.

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.", inaeleza Biblia katika chake (Yohana 3:16 )

Siku ya Krismasi ni fursa ya kutulia na kushukuru kwa upendo, tumaini na furaha inayopatikana katika Yesu

‘’Tunapobadilishana zawadi na wapendwa wetu, ni kwa ukumbusho wa zawadi ambayo Mungu alitupa katika Yesu. Zawadi ambayo tunapendwa, hatuko peke yetu na tunaweza kuwa na tumaini la siku zijazo’’, anasema mmoja wa viongozi dini ya Kikristo.

Kupeana zawadi za Krismasi pia ni kumbukumbu ya zawadi ambazo alipewa Yesu Kristo baada ya kuzaliwa, kulingana na Biblia. Baada ya Yesu kuzaliwa, kikundi kidogo cha mamajusi kilimtembelea. Walitambua ufalme wa Yesu na “wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi za dhahabu, uvumba na manemane” (Mathayo 2:11).

Katika kipindi hiki Wakristo wanahimizwa pia, ibada na shukrani kwa Mungu kupitia maombi Krismasi. Maombi ya shukrani kwa zawadi ya tumaini, upendo na furaha.

Shughuli nyingi za kuwatembelea wagonjwa na kutoa misaada mbali mbali kama vile mavazi na chakula hushuhudiwa zaidi katika msimu wa Krisimasi kama ishara ya kuonyesha upendo kwa binadamu- mfano aliouonyesha Mungu na Yesu Kristo kwa binadamu.

Kulingana na Wakristo Siku ya Krismasi ni fursa ya kutulia na kushukuru kwa upendo, tumaini na furaha inayopatikana katika Yesu