Maelezo zaidi yameendelea kuibuka kuhusu mshukiwa wa mauaji ya mfululizo John Matara, ambaye amekuwa akivuma baada ya kuhusishwa na kifo cha mwanasosholaiti Starlet Wahu.
Matara ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji ya dadake Prohet Victor Kanyari mwenye umri wa miaka 26 ambaye mwili wake ulipatikana Alhamisi wiki jana katika chumba cha Air BnB eneo la South B, Nairobi. Alikamatwa katika hospitali ya Mbagathi akitafuta matibabu baada ya kupata majeraha kadhaa.
Kufikia sasa, tumefaulu kukusanya maelezo fulani kuhusu mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 34, ambayo baadhi yake ni ya kushtua na kufichua unyama ndani ya mwanafunzi huyo wa zamani wa Shule ya Upili ya Wavulana ya Butere.
Hapa kuna maelezo kadhaa kuhusu John Matara;
- Jina lake halisi ni John Ongoa Matara
- Ana umri wa miaka 34
- Alisoma katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Butere
- Anatoka Kaunti ya Kisii
- Aliwahi kuwa msanii wa reggae kwa jina - Rebelius Monk
- Ana wimbo uitwao ‘Time has Proven’ kwenye YouTube
- Anawahadaa na kuwatapeli/kuwaibia pesa wahasiriwa wake wa kike
- Matara aliwaambia polisi kuwa yeye ni mbunifu wa michoro
- Alidaiwa kuwa mtumiaji wa kawaida wa Bangi
- Wakati fulani alikuwa Rastafari
- Anapata wahasiriwa wake kutoka kwa programu za uchumba
- Matara alikamatwa katika Hospitali ya Mbagathi pamoja na rafiki yake Anthony Nyongesa. Anaendelea kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Industrial Area.
- Ndiye mshukiwa mkuu wa mauaji ya Starlet Wahu
- Mshukiwa anaweza kuwa muuaji wa mfululizo na mnyang'anyi.
- Polisi wanamshikilia kwa siku 21 ili kuruhusu uchunguzi zaidi.
- Kufikia sasa waathiriwa watatu wamerekodi taarifa na polisi.
- Wanaowezekana kuwa waathiriwa wengine wameendelea kufichua matukio yao naye kwenye mitandao ya kijamii.
HISANI: DCI, polisi, utafiti mitandaoni, kukiri kwa waathiriwa, hati.