Siku ya Kondomu duniani: Kondomu za kike zinalingana na zile za kiume kwa usalama, lakini hazitumiki

Kondomu za wanawake zina uzuri wake – kumfanya mwanamke kudhibiti kinachoendeleea.

Muhtasari

• Maswala ya sayansi, majukumu ya kijinsia, na tofauti katika uwezo wa raslimali huwafanya wanawake kukabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa yanayotokana na ngono.

• Takwimu zinaonyesha kuna haja ya kuanzishwa mazungumzo kuhusu matumizi ya Kondomu za wanawake.

Kondomu ya wanawake
Kondomu ya wanawake
Image: Maktaba

Licha ya viwango vya juu vya maambukizi ya virusi vya Ukimwi (HIV) miongoni mwa wanawake kote duniani, mipira ya kodomu iliyoundwa maalum kutumika na wanawake inasambazwa kwa kiwango cha asilimia 1.6 ikilinganishwa na kiwango cha jumla cha usambazaji wa kondomu zote zikiwemo za kutumika na wanaume. 

Siku ya Mipira ya Kondomu duniani huadhimishwa kila tarehe 13 ya mwezi Februari, siku hii ikitengwa kwa kuhimiza watu watumie mipira ya Kondomu ili kufanya mapenzi ambayo ni salama.

Na ulimwengu ukiadhimisha siku hii, takwimu zinaonyesha kuna haja ya kuanzishwa mazungumzo kuhusu matumizi ya Kondomu za wanawake.

Ikitajwa kuwa mipira ya Kondomu ya kuingizwa ndani, kondomu za wanawake zina uzuri wake – kumfanya mwanamke kudhibiti kinachoendeleea. Ikilinganishwa na Kondomu za wanaume, Kondomu za wanawake zinawapa uwezo za kuwajibikia afya yao kuhusiana na maswala ya mapenzi.

Maswala ya sayansi, majukumu ya kijinsia, na tofauti katika uwezo wa raslimali huwafanya wanawake kukabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa yanayotokana na ngono. Wengi hawana elimu kuhusu afya ya uzazi na namna ya kujilinda. 

Hata hivyo, kuwaelimisha wanawake kuhusu matumizi ya kondomu za wanawake kunawapa uwezo wa kujikinga kutokana na maambukizi na hata kushauriana kwanza na wapenzi juu ya matumizi ya Kondomu kwa ajili ya usalama wao.

Hili likifanyika, mwanamke anajikinga kutokana na kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na HIV, na Kaswende na Kisonono.  

Image: Maktaba

Utafiti unaonyesha kwamba mipira ya kondomu ya wanawake ina uwezo wa kuzuia maambukizi ya HIV kwa kiwango cha asilimia 94 ikitumika ipasavyo wakati wa ngono, ikilinganishwa na kondomu ya wanaume ambayo inazuia HIV kwa kiwango cha asilimia 90.

Hofu kuu ya kutumika kwake, ama kutozea kutumia, ndio hufanya watu wengi kukosa kufikiria kuitumia. Ili hali kondomu za wanawake zinaweza kutumika vizuri sana. Kondomu hii inatiwa katika sehemu ya uzazi ya mwanamke saa chache kabla ya tendo la ngono, na wahusika wakizoea kuitumia, basi inakuwa ni rahisi sana kutumika.

Kadhalika, kupatikana kwa kondomu za wanawake pia ni changamoto iliyo wazi kwani unapoenda madukani, sio rahisi uipate pale. Mashirika yasio ya serikali na isara chache za serikali ndio walio na kondomu za wanawake, huku zikikosekana katika sehemu muhimu kama vile maduka ya dawa maduka ya bidhaa na maduka ya jumla. 

Serikali inaweza kuhakikisha kondomu za wanawake zinapatikana kila mahali kupitia kwa mipango ya elimu juu ya afya ya uzazi, kupeane ile mipira bila malipo ama kwa malipo ya chini, na mwisho kuanzisha kampeini inayolenga kumaliza uoga wa kutumia kondomu za wanawake. Pia, ununuzi wa mipira hii ukijumlishwa katika sera za serikali za kununua bidhaa, itasaidia kuona kwamba mipira hio ya kondomu za wanawake inapatikana na kutumika kwa urahisi.

Japokuwa ni muhimu ijulikane kwamba mipira ya kondomu ya wanawake huenda ikawa haipendelewi na wengi, lakini dhana hio inaweza kubadilishwa pole pole. 

Kwa ufupi, kuhimiza kupatikana rahisi na kutumika kwa kondomu za wanawake kutasaidia wanawake kujikinga na magonjwa. Ni mbinu ya kuwapa uwezo wanawake, ili wajiamulie juu ya mambo yanayowahusumu moja kwa moja ya kushiriki mapenzi, lengo kuu likiwa kuhakikisha usalama na afya kwa wote.

Mwandishi wa maoni haya, Oluwakemi Gbadamosi, ni mkurugenzi wa utetezi, sera na masoko katika wakfu wa AIDS Healthcare barani Africa.