Fahamu kuhusu Jiji la Fatima linalotembelewa sana na Wakristo kutoka kote duniani

Hata Papa Francis alikwenda katika mji huo Mei 2017, miaka 100 baada ya kumbukumbu ya Maria.

Muhtasari

•Takriban maili 40 kaskazini mwa Lisbon, jengo la Fátima sasa ni jengo kubwa, lenye hadithi na vyombo vingine vitakatifu.

•Mahujaji Wakatoliki huenda katika kijiji cha Fatima kutoka mbali kama vile China, Venezuela na Timor ya Mashariki.

Image: BBC

Zaidi ya karne moja iliyopita, kijiji cha Fatima katikati mwa nchi ya Ureno kilikuwa eneo la mashambani lililoshiriki sana katika ufugaji wa kondoo.

Leo, ni sehemu kuu ya ibada au vinginevyo hija ya Kikatoliki.

Santuário de Fátima, iliyojengwa mwaka wa 1917 kama mahali pa kukutania kwa ndoto na miujiza, huvutia wageni milioni 9.4 kwa mwaka.

Hata Papa Francis alikwenda katika mji huo Mei 2017, miaka 100 baada ya kumbukumbu ya Maria.

Takriban maili 40 kaskazini mwa Lisbon, jengo la Fátima sasa ni jengo kubwa, lenye hadithi na vyombo vingine vitakatifu ambavyo vilikamilishwa mwaka wa 2007 - na kulifanya kuwa Kanisa Katoliki la nne kwa ukubwa duniani.

Muujiza wa Maria

Maelezo ya picha,Papa Francis alipotembelea jiji hilo hivi karibuni
Maelezo ya picha,Papa Francis alipotembelea jiji hilo hivi karibuni
Image: BBC

Ilikuwa mwezi Mei 13, 1917 ambapo Marekani ilikuwa imejiunga na washirika wake katika Vita vya kwanza vya Dunia. Wakati huohuo, watoto watatu - Lucia dos Santos mwenye umri wa miaka 10 na binamu zake Jacinta Marto, 7, na Francisco Marto, 8 - walikuwa wakiwachunga na kuwapeleka katika lishe kondoo wa jamaa zao.

Wachungaji hao watatu wachanga mara ghafla waliona mwanga mkali katika mahali paitwapo Cova da Iria, katika kijiji cha Fatima karibu na Lisbon. Mwanga huo ulimuonesha msichana anayeangaza kama jua.

Msichana huyo aliyesimama alizungumza na mmoja wa wasichana wadogo, Lucia na alijitambulisha kama Mama Yetu wa Rozari na akamwambia Lucia kwamba angerudi katik aeneo hilohilo miezi 13 ijayo.

Kila mwezi, watoto walikuwa wakirudi kwenye eneo hilo na kumwona msichana, ingawa hakuna mtu mwingine angeweza kumuona.

Na hapa ndipo hadithi nyingi za miujiza ambazo Wakatoliki wanaamini zimetoka.

Image: BBC

Kanisa Katoliki linatoa umuhimu wa pekee kwa yale wanayosema ni mafumbo matatu ya Mariamu - msichana aliyesimama pale na kuwaona watoto wachungaji na kuzungumza nao .

Kanisa Katoliki, lilieleza mafumbo hayo matatu kuwa ni unabii kuhusu mwisho wa matukio.

Matukio hayo yaliangazia siri kuhusu kuzimu na maovu yake, unabii kuhusu mwisho wa Vita vya Kwanza vya dunia na mwanzo wa Vita vya vya pili vya dunia, na siri ya tatu ilifasiriwa kuwa inatabiri wa jaribio la kumuua Papa Yohane Paulo II Mei 13, 1981

Baba wa kanisa hilo anafikiri kwamba habari hii ilikuwa 'ufunuo' uliyokusudiwa kuboresha maisha ya watu.

Hajj ya Fatima

Mahujaji Wakatoliki huenda katika kijiji cha Fatima kutoka mbali kama vile China, Venezuela na Timor ya Mashariki.

Hajj ya kwanza ilikuwa mwaka 1927, 1928 ambapo Lucía dos Santos baadaye alikuwa mtawa katika nyumba ya watawa ambako alifikia umri wa karibu miaka 97.

Hatahivyo Francisco na Jacinta Marto, wasichana wawili walioandamana naye kuona muujiza huo, walikufa utotoni kwa sababu ya mlipuko wa mafua uliotokea kati ya miaka ya 1918-1919.

Baadaye Lucia dos Santos, aliyefariki mwaka wa 2005, aliandika kitabu kiitwacho Siri Tatu za Fatima.