Mambo manne yanayoweza kusababisha kifo cha ghafla kwa binadamu

Moyo wa mtu ukishindwa kufanya kazi kwa kawaida husababisha kifo cha ghafla.

Muhtasari

•Vitu vinavyosababisha pumzi kutokuwa sawa kama inavyotatikana ni inaweza kuwa pengine matumizi ya dawa za kulevya, magonjwa ya moyo.

•Ikiwa damu haifiki sehemu ya ubongo, mtu atapata ugonjwa wa kupooza.

Image: BBC

Ingawa kila mtu aliyepo dunia anajua kwamba siku moja atafariki dunia, bado hakuna anayetaka kufa kifo cha ghafla.

Ndio maana inashangaza tunaposikia kifo cha mtu ambaye pengine alikuwa mzima lakini akafariki kwa namna hiyo.

Ikiwa mtu ambaye ni mzee atafariki dunia kuna wale ambao utasikia wakisema, labda alikuwa amekula chumvi nyingi lakini mtazamo hauwezi kuwa hivyo atakapokuwa kijana.

Lakini kifo hakina uhusiano wowote na umri, kwa sababu watoto pia hufariki

Aina hii ya kifo huchukuliwa kuwa ghafla.

Daktari Adamu Mohammed ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo aliieleza BBC kwamba moyo wa mtu ukishindwa kufanya kazi kwa kawaida husababisha kifo cha ghafla.

Daktari kutoka Chuo Kikuu cha Usman Danfodiyo, katika jimbo la Sokoto aliorodhesha mambo manne yanayosababisha kifo cha ghafla.

Kushindwa kupumua inavyotakikana

Image: BBC

Kuna ugonjwa unaotatiza moyo unaojulikana kama 'arrhythmia'.

Unaweza kufanya moyo kupiga haraka sana au polepole sana.

Nafsi ya mtu ambaye anasumbuliwa na tatizo hili itafadhaika.

Moyo wa mtu unapofanya kazi, unaweza kupiga kwa haraka sana mtu anapokuwa kwenye michezo na kupunguza kasi anapomaliza.

Vitu vinavyosababisha pumzi kutokuwa sawa kama inavyotatikana ni inaweza kuwa pengine matumizi ya dawa za kulevya, magonjwa ya moyo na hufanya mwili kushindwa kabisa kufanya kazi.

''Mambo madogo madogo yanaweza kuchangia mioyo kuwa katika matatizo. Hata hivyo, ikiwa yataendelezwa kwa muda yanaweza kuathiri utendaji wake kiafya.

"Hii inaweza kusababisha akili zao kuacha kufanya kazi, na ikiwa akili itaacha kufanya kazi, kifo cha ghafla kitatokea," Dk Adamu alisema.

Ikiwa damu haifiki kwa moyo wa mwanadamu

Kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye moyo kutasababisha oksijeni kidogo kufikia moyo.

Ikiwa hii itatokea, damu itapita juu ya ngozi.

Kwa mujibu wa Dk Adamu, sababu ni uvutaji wa sigara, kisukari, upungufu wa damu, mzunguko wa kawaida wa damu, kutofanya mazoezi mara kwa mara, mshtuko wa ghafla na matumizi ya dawa za kulevya.

Damu kutofika sehemu ya ubongo

Image: bbc

Ikiwa damu haifiki sehemu ya ubongo, labda kwa sababu mishipa ya damu imefungana au kwa sababu nyengine yoyote ile, mtu atapata ugonjwa wa kupooza.

Hii ndio uitwa kiharusi.

Ugonjwa huu kawaida huua maeneo fulani katika ubongo wa mwanadamu.

Ikiwa mtu hatapata matibabu sahihi mapema, anaweza kuishia kutumia dawa za matibabu ya ubongo.

Baadhi ya mifano ya kupooza ni kwamba mtu hawezi kuongea vizuri, kutapika wakati ulemavu unakaribia kutokea, mtu hawezi kusikia kile watu wanachozungumza, au hata kuona vizuri.

Haya yote yanaweza kusababisha kifo cha ghafla.

Mapafu yakifungana

Image: BBC

Kinachosababisha hali hii ni iwapo misuli itashindwa kufanya kazi miongoni mwa ile inayosukuma damu mwilini, hasa miguuni.

Damu ambayo haiwezi tena kusambaa mwilini itaenda kwenye mapafu, na mapafu yatashindwa kufanya kazi.

Ikiwa hii itatokea, oksijeni ambayo mapafu husukuma mwilini itaacha kufanya kazi.

Inaweza kusababisha moyo kuacha kufanya kazi, na hata kuingilia kati jinsi damu inavyopita kwenye moyo.

Ikiwa matibabu ya haraka hayapatikani, inaweza kusababisha kifo cha ghafla.

Ripoti moja inasema kuwa mtu mmoja kati ya watatu wanaokumbwa na tatizo hili hufariki dunia.

Mtu anaweza kushindwa kupumua vizuri, moyo ukawa ni wenye kupiga kwa haraka mno kuliko inavyopaswa. Yote hii ni hatari sana kwa binadamu na ndiyo maana madaktari wanasema kwamba watu ambao wana ugonjwa wa moyo hawawezi kuachwa peke yao.

Wanahitaji huduma wakati wowote ule.

Jinsi ya kuzuia kifo cha ghafla

Yeyote anayekabiliwa na matatizo yaliyoelezwa na Dkt. Adamu anatakiwa kwenda hospitali haraka iwezekanavyo.

Lakini kabla ya kwenda hospitali, mtu huyo anahitaji kwanza matibabu ili kurejesha moyo wake uliozimia.

Profesa Kamilu Musa Karaye ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Chuo Kikuu cha Mallam Aminu Kano, katika jimbo la Kano, aliambia BBC kwamba waliokuwa na mtu huyo lazima wahakikishe kuwa bado anapumua.

Akiongeza kuwa mtu anayejua kuhusu mchakato wa kusukuma moyo ili uwanze tena kufanya kazi, wanastahili kufanya hivyo tena na tena hadi wafike hospitalini.