Siku ya Jumatano, Mmarekani mwenye asili ya Kenya, Huldah Momanyi Hiltsley aliweka historia kubwa kwa kunyakua kiti katika Baraza la Wawakilishi la Minnesota.
Ushindi huo wa mzaliwa wa kaunti ya Nyamira ulimfanya kuwa mwanasiasa wa kwanza mzaliwa wa Kenya kushinda kiti nchini Marekani.
Momanyi alishinda kwa 64.78% ya kura kuwakilisha Wilaya ya 38A ya Minnesota huku akigombea chini ya tiketi ya Chama cha Democratic-Farmer-Labor (DFL).