logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Njia 8 za kuwa na furaha zaidi mwaka huu

Hapa kuna vidokezo vyetu vikuu vya kuufanya mwaka 2025 uwe wenye furaha zaidi kwako

image
na BBC NEWS

Makala03 January 2025 - 16:07

Muhtasari


  • Urafiki huwanufaisha watu wa umri mbalimbali, lakini uzeeni unaweza kuwa chanzo muhimu zaidi cha furaha.

g

Watu wengine wamezaliwa kuwa na furaha kuliko wengine. Lakini uwe ni aina ya watu ambaye huimba bafuni wakati wa na kucheza kwenye mvua, au ni wa mwelekeo wa huzuni zaidi, kuridhika si kitu kinachotokea bila kutarajia. Sote tunaweza kubadilisha tabia zetu ili kufikia furaha zaidi katika maisha yetu.

Hapa kuna vidokezo vyetu vikuu vya kuufanya mwaka 2025 uwe wenye furaha zaidi kwako:

Kuzingatia urafiki tunapozeeka

Urafiki huwanufaisha watu wa umri mbalimbali, lakini uzeeni unaweza kuwa chanzo muhimu zaidi cha furaha.

Ingawa watu wazee mara nyingi hupunguza mizunguko yao ya kijamii ili kutanguliza kutumia wakati na wale wanaowajua vizuri, utafiti unaonyesha kuwa ni wazo zuri kuwa wazi kwa urafiki mpya, kwani hutupatia faida tofauti kidogo kuliko uhusiano wetu wa kifamilia - ambao unaweza kujengwa juu ya majukumu.

Kwa sababu urafiki ni wa hiari, si wa lazima, uhusiano ambao unaweza kuanza au kumalizika wakati wowote, huwa na furaha zaidi na usio na wasiwasi au wenye matatizo.

Ingawa watu wazima wanaweza kukabili vikwazo kadhaa vinavyoweza kufanya kukutana na watu wapya kuwa vigumu, kwa njia fulani inapaswa kuwa rahisi kwetu kupata marafiki: haiba zetu zinakomaa, tunapata ujuzi zaidi wa kijamii, mtazamo wetu unakuwa mzuri zaidi, na tunaelekea kuungana na kila mmoja anapofanya hivyo ifurahisha zaidi.

Na juhudi za kudumisha urafiki wa hali ya juu kadri tunavyozeeka zinafaa, kwani faida hupita zaidi ya ustawi wa kisaikolojia na pia huboresha utendaji wetu wa utambuzi na afya ya mwili.

Kwakweli, utafiti mara kwa mara unapendekeza kwamba urafiki ni muhimu kama vile uhusiano wa familia katika kutabiri ustawi miongoni mwa watu wazima na uzee.

Na kama wewe ni aina ya mtu ambaye ni vigumu kupata marafiki, kushiriki tukio la kupendeza, kama vile kupatwa kwa jua kwa jumla kulikopita Amerika Kaskazini mwaka jana, ni njia mojawapo ya kukusaidia kujisikia karibu na watu walio karibu nawe na, wakati huo huo, kuhamasisha baadhi ya hisia chanya.

Fanya mazoezi ya 'furaha'

g

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Inaaminika kuwa kutazamia shughuli za kujifurahisha kunaweza kutupa mtazamo wenye matumaini zaidi

Huruma ni msingi unaojulikana sana wa urafiki wa kweli. Imetoka kwa Kilatini kwa "maumivu ya pamoja," huruma hii hutusaidia kuunda miunganisho thabiti wakati marafiki zetu wanapohitaji usaidizi. Lakini kuna hali tofauti ambayo haijulikani na ni muhimu vile vile - uaminifu , kama David Robson alivyoandika kwenye makala ya BBC , neno kwa Kiingereza ambalo linaweza kutafsiriwa kama "confliciness".

Kumaanisha "furaha ya pamoja", ni sehemu isiyothaminiwa ya mahusiano mazuri na inaweza kuwa muhimu kama huruma katika kudumisha urafiki, tafiti kadhaa zinaeleza.

Kuunga mkono kwa shauku habari njema za rafiki na kuuliza maswali kuzihusu ndio msingi wa kuwa rafiki mzuri. Kujibu kwa utulivu sana au kuzuia mafanikio ya rafiki yako kunaweza kuharibu uhusiano.

Fanya kazi ya kujitolea

Ni karibu maneno machache kusema kwamba kufanya kitu kwa ajili ya mtu mwingine hukufanya ujisikie bora kuliko kujithawabisha, lakini kadiri unavyojifunza zaidi kuhusu kujitolea, ndivyo hii inavyoonekana kuwa kweli.

Kwakweli, tafiti zimegundua kuwa kujitolea kunaweza kusaidia hata kwa magonjwa makali kama maumivu sugu na unyogovu. Uchunguzi wa 2002 wa watu wanaosumbuliwa na maumivu ya kudumu, kwa mfano, uligundua kwamba wale waliojitolea kusaidia wengine wanaosumbuliwa na maumivu ya muda mrefu waliona alama zao za maumivu zinapungua wakati wa kazi yao ya kujitolea.

Uchunguzi mwingine umeonyesha kwamba kutunza wanyama kunaweza kuboresha afya zetu na kutunza mimea ya ndani kunaweza kutusaidia kustawi, hasa katika uzee.

Baadhi ya watoa huduma za afya sasa hata wanaagiza kujitolea kama aina ya ufanisi hasa ya "maagizo ya kijamii": ambayo inaunganisha watu kwa rasilimali na shughuli za jumuiya.

Shughuli zinazopendekeza watu kama vile madarasa ya sanaa au vikundi vya baiskeli au densi ni shughuli za kiafya ambazo zinazidi kuthibitishwa kuwa halali na pia zinaweza kupunguza shinikizo kwa huduma za afya ya umma.

Kuungana na mababu zako

Kuna njia nyingine ambayo ni ya wakati uliopita inayoweza kusaidia sasa.

Utafiti unapendekeza kwamba kujihusisha na mababu zetu kunaweza kuwa na manufaa makubwa ya kisaikolojia. Hadithi za familia kuhusu kushinda dhiki, kwa mfano, zinaweza kutia nguvu zinapopitishwa kwa kizazi kijacho.

Susan M. Moore, profesa wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Swinburne huko Melbourne, Australia, aligundua kwamba watu wanaojua zaidi kuhusu historia ya familia zao wana viwango vya juu vya kuridhika na hali njema.

Kujihusisha na kazi ya utafiti wa mizizi ya familia kunaweza kuwaacha watu wakijihisi kuwa na udhibiti zaidi wa maisha yao, pamoja na ufahamu wa kina wa nafasi yao duniani.

Inaweza pia kukupa hisia chanya ya mtazamo na shukrani, ukijua kwamba maisha yako ya sasa yaliwezekana kwa mapambano na ujasiri wa watangulizi wako kwa niaba ya wale waliokuja baada yao.

g

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Kufurahia bahati ya marafiki zetu ni muhimu kudumisha uhusiano mzuri pamoja nao

Andika orodha

Kuwa na shukrani kwa kile ulicho nacho ni ushauri wa kale, linapokuja katika suala la kuwa na furaha.

Inajulikana kuwa kuandika orodha ya mambo matatu mazuri yaliyotupata kunaweza kusaidia kuboresha hisia zetu.

Iwe ni tukio la kubadilisha maisha kama vile kufaulu mtihani muhimu au kupata mtoto, au jambo linaloonekana kuwa la kawaida kama vile kukutana na rafiki wa zamani au kufurahia mwangaza wa jioni wakati wa kutembea, kuna kundi kubwa la utafiti linalopendekeza kwamba linaweza kuboresha hisia zetu.

Furahia matarajio ya shughuli za kufurahisha

Watafiti katika chuo kikuu cha Richmond huko Virginia walifundisha panya-wa kufugwa kuendesha magari madogo ya Perspex kwenye maabara.

Panya hao walifaulu ustadi huu mpya haraka na punde wakawa wanaruka kwenye magari kwa msisimko wakijitayarisha kwa safari inayofuata. Hatimaye, watafiti waligundua kwamba panya wengine waliruka kidogo, na msisimko, kana kwamba walikuwa wakifurahia kutarajia raha.

Hii ilisababisha njia mpya ya utafiti. Je, matarajio ya furaha yanaweza kuwa yenye kuridhisha kama shughuli yenyewe?

Katika jaribio lingine, wanasayansi waliwazoeza baadhi ya panya kusubiri zawadi, huku wengine wakizipokea mara moja. Baadaye walitathmini matumaini ya panya hao na wakagundua kwamba wale waliokuwa wamezoezwa kungoja zawadi walikuwa na matumaini zaidi.

Watafiti walikisia kuwa hii inaweza kufanya kazi kwa wanadamu pia kwa kutarajia shughuli au matukio ya kupendeza mara kwa mara, tunaweza kurekebisha akili zetu kuwa na matumaini zaidi.

Usifanye chochote

Ikiwa umeifanya iwe chini kabisa kwenye orodha, hii inaweza kukushangaza. Lakini utafiti unapendekeza kwamba kuhangaikia sana furaha kwa kweli kunaweza kuwa kikwazo cha kuihisi.

Majaribio ambayo yaliwahimiza watu kutamani furaha zaidi - labda kwa kusoma kuhusu jinsi wanavyoweza kuwa na furaha - kabla ya kutazama filamu ya kusisimua au ya kuinua yaligundua kwamba waliishia kuvunjika moyo zaidi kuliko kufurahishwa.

Nadharia ni kwamba kwa kuongeza matarajio, kusoma na kuwa na wasiwasi juu ya umuhimu wa furaha kwa kweli kunaweza kuwafanya watu wahisi kukata tamaa.

Labda umejionea haya mwenyewe wakati wa hafla kubwa au tafrija ambayo ulikuwa ukitarajia na ambayo haikuafiki matarajio.

Iris Mauss, mwanasaikolojia katika chuo Kikuu cha California, Berkeley, pia ameonyesha kwamba tamaa na utafutaji wa furaha unaweza pia kuongeza hisia za upweke na kukatwa. Anapendekeza kuwa na mtazamo wa kukubali zaidi heka heka za maisha.

g

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Kujaribu sana kuwa na furaha kunaweza kuwa na madhara kwa ustawi wetu

Usinywe kafeini nyingi

Wakati wa baridi, siku za baridi kali, kikombe cha kahawa kinaweza kuupa ubongo na mwili wako msukumo unaohitajika sana.

Kunywa kafeini kunaweza kutufanya tujisikie macho kwa sababu inafyonzwa haraka kwenye mfumo wa damu, ambapo inapita adenosine, kemikali ambayo hutufanya tuhisi uchovu.

Utafiti unaonyesha kuwa kuna faida nyingi za kiafya zinazohusiana na matumizi ya kafeini, ikiwa ni pamoja na kupunguza hatari ya aina mbalimbali za saratani, ugonjwa wa moyo na kisukari cha aina ya 2, pamoja na kuboresha utendaji wa kimwili na ulinzi dhidi ya huzuni.

Lakini muda ni muhimu linapokuja suala la kafeini, kwani inaweza kuchukua muda kuanza kutumika na muda mrefu kuisha.

Wanasayansi wanapendekeza kuchukua dozi yako ya mwisho ya kafeini saa nane na dakika 48 kabla ya kwenda kulala.

Pia hatupaswi kutumia kafeini nyingi - si zaidi ya miligramu 400 au vikombe viwili hadi vitatu vya kahawa, kulingana na nguvu - ili kuepuka usumbufu wa usingizi, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na wasiwasi.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved