logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nyota adimu inaweza kuonekana kwa mara ya kwanza katika miaka 160,000

Nasa ilisema mng'ao wa siku zijazo wa nyota hiyo "ni vigumu sana kutabiri," lakini inaweza kuendelea kung'aa vya kutosha kuonekana kwa macho.

image
na BBC NEWS

Makala14 January 2025 - 07:13

Muhtasari


  • Nyota angavu ya Comet C/2024 G3 inaweza kuonekana angani kote ulimwenguni katika siku zijazo kwa mara ya kwanza katika miaka 160,000.

.

Chanzo cha picha,Don Pettit/NASA

Maelezo ya picha,Nyota hiyo ilionekana kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga cha Juu mwishoni mwa juma

Nyota angavu ya Comet C/2024 G3 inaweza kuonekana angani kote ulimwenguni katika siku zijazo kwa mara ya kwanza katika miaka 160,000.

Nasa ilisema mng'ao wa siku zijazo wa nyota hiyo "ni vigumu sana kutabiri," lakini inaweza kuendelea kung'aa vya kutosha kuonekana kwa macho.

Siku ya Jumatatu, nyota hiyo ilikuwa kwenye ‘Periheli’ mahali katika obiti ya sayari ambako ni karibu zaidi na jua, kunakochangia jinsi inavyoonekana yaani yenye kung’aa sana.

Wataalam wanasema inaweza kuonekana kuanzia Jumatatu usiku.

Ingawa maeneo kamili ya uwezekano wa kuonekana hayajulikani, wataalam wanaamini kwamba nyota Comet, ambayo inaweza kung'aa kama sayari ya Zuhura, itakuwa vizuri zaidi kuitazama kutoka upande wa Kizio cha Kusini.

Dk Shyam Balaji, mtafiti wa fizikia ya astroparticle na cosmology katika Chuo cha King's College London, alisema "hesabu za sasa za obiti zinaonyesha kuwa itapita takriban maili milioni 8.3 kutoka kwenye Jua".

Bw Balaji aliwashauri watu wanaotaka kuona nyota hiyo kutafuta eneo lililo mbali na uchafuzi wa mwanga na kutumia jozi ya darubini au darubini ndogo.

Aliwaonya waangalizi kuwa waangalifu wakati jua linachomoza na machweo, na kuongeza kuwa wafuatilie ili wajue mahali ambapo inaweza kuonekana angani.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved