logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaume amuua mwanawe wa kambo wa miaka 3 kulipiza kisasi baada ya kutengana na mamake

Senkanjako Vincent anasemekana kufanya kitendo hicho mbovu mnamo Machi 26, 2024 na kutoroka.

image
na Davis Ojiambo

Habari04 April 2024 - 08:28

Muhtasari


  • Siku iliyofuata, inasemekana Vincent alimfuata Nakintu kwa nia ya kurudiana na kumsihi arudi nyumbani.
crime scene

Polisi katika Wilaya ya Wakiso, Uganda ya Kati, wameanzisha msako kumsaka mwanamume mwenye umri wa miaka 40 anayedaiwa kumuua mtoto wake wa kambo wa miaka 3 ili kulipiza kisasi kufuatia kutengana na mama wa mtoto huyo.

Senkanjako Vincent anasemekana kufanya kitendo hicho mbovu mnamo Machi 26, 2024 na kutoroka.

Ripoti ya polisi inasema kwamba Vincent na mkewe Nakintu Faith Florence walikuwa wakiishi kama familia lakini walitengana baada ya mke wake kugundua kuwa aliiba simu ya rununu, runinga na UGx 100,000 kutoka kwa nyumba yao.

"Nakintu alilazimika kuondoka nyumbani na mtoto wake wa kiume wa miaka 3 na kwenda kukaa na rafiki yake katika Kituo cha biashara cha Temangalo", Ripoti ya polisi inasema.

Siku iliyofuata, inasemekana Vincent alimfuata Nakintu kwa nia ya kurudiana na kumsihi arudi nyumbani.

"Wakati wa mchakato huo, alikwenda na mtoto wake wa kambo, kwenda kununua soda, lakini alitoweka naye. Mama alipata wasiwasi, saa 10 jioni, baada ya kuwasubiri bila mafanikio. upekuzi ulifanyika," ripoti hiyo inaongeza.

Kisha mwili wa mwathiriwa ulipatikana kwenye chumba karibu na nyumba yao ukiwa na majeraha mabaya kichwani yaliyotokana na kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo cha papo hapo.

“Uhalifu mkubwa namna hii unapofanyika inaonyesha hatari ambayo bado watoto waishio katika mazingira magumu bado wanakumbana nayo katika jamii yetu, tunakwenda kuweka juhudi zetu, kumsaka mtuhumiwa na kuhakikisha anafikishwa mbele ya haki, hatutakoma hadi amekamatwa", msemaji wa polisi wa Uganda Enanga Fred alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved