Picha ya siku!Tazama jinsi Eric Omondi alivyojifungia ndani ya mchemraba nje ya Bunge

Muhtasari
  • Wanaume sita waliovalia suti nyeusi, inaonekana walinzi wake, wanazunguka mchemraba huo
Eric Omondi
Image: Julius Otieno

Mcheshi Eric Omondi amejifungia ndani ya 'mchemraba wa uwazi' nje ya majengo ya bunge katika juhudi za kuwashawishi wabunge kujadiliana kuhusu kuongeza uchezaji wa hewani na maudhui.

Anasema wabunge wanapaswa kuhakikisha hadi asilimia 75 ya muziki na kazi nyingine za kisanii zinazochezwa kwenye TV na redio za Kenya ni maudhui ya ndani.

“Nitabaki hapa hadi watakapoanza mjadala huu ni mgomo wa kula,” alisema.

Wanaume sita waliovalia suti nyeusi, inaonekana walinzi wake, wanazunguka mchemraba huo.

Hizi hapa baadhi ya picha za mcheshi huyo;

Image: Julius Otieno
Image: JUlius Otieno