(Video) Nairobi! Jamaa avunja gari na kuiba shilingi milioni 1.4 mchana peupe

Muhtasari

•Mshukiwa huyo anaripotiwa kumfuata mhasiriwa kutoka benki moja katika mtaa wa Industrial Area hadi mtaa wa Kamukunji ambapo wizi huo ulifanyika.

Image: HISANI

Polisi jijini Nairobi wanamsaka jamaa mmoja aliyenaswa na CCTV akivunja gari ndogo na kuiba kitita kikubwa cha pesa.

Katika kanda ya video ya CCTV inayoenezwa mitandaoni, mwanaume mwenye umri wa wastani aliyekuwa amevalia shati ya zambarau na suruali nyeusi alionekana akivunja gari ya bluu  na kuchukua kibahasha kinachoripotiwa kuwa na pesa taslimu Sh 1.4M.

Mshukiwa huyo anaripotiwa kumfuata mhasiriwa kutoka benki moja katika mtaa wa Industrial Area hadi mtaa wa Kamukunji ambapo wizi huo ulifanyika.

Kamera za CCTV  zilimnasa mshukiwa akifanya majaribio kadhaa ya kuvunja gari hilo na hatimaye akafaulu. Video hiyo inaonyesha mshukiwa akitafuta mahali pesa zimewekwa na hatimaye anaonekana akiondoka na kijibahasha kilichojaa pesa.

Tazama hapa:-