(Picha) Mwanasiasa atembea mtaani mguu tupu akiwa amevalia kaptura katika juhudi za kutafuta kura

Muhtasari

•Kwa vile chama hicho kinadai  kuegemea upande wa mwananchi wa kawaida (Hustler) , Theuri hajasazwa nyuma katika juhudi za kumuiga raia wa kawaida.

Image: FACEBOOK// GEORGE THEURI

Huku kampeni za uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti zikiwa zimenoga katika maeneo mbalimbali ya nchi, wanasiasa wamekuwa wabunifu sana na mbinu tofauti za kuwarubuni wapiga kura.

Nyakati kama hizi ndizo wagombeaji wa viti tofauti hujaribu kuyaiga maisha ya mwananchi wa kawaida katika juhudi za kuwashawishi wawapigie kura.

George Theuri ni mgombeaji wa kiti cha ubunge cha Embakasi Magharibi kwa tikiti ya chama cha Ruto, UDA.

Kwa vile chama hicho kinadai  kuegemea upande wa mwananchi wa kawaida (Hustler) , Theuri hajasazwa nyuma katika juhudi za kumuiga raia wa kawaida.

Siku ya Jumanne mwanasiasa huyo alipakia picha zake akiwa kwenye pilkapilka za kampeni katika eneo bunge la Embakasi.

"Napenda kila dakika mtaani," Theuri aliandika chini ya picha zake akiwa mguu tupu huku akiwa amevalia kaptura na jezi ya manjano ya soka yenye maandishi 'Theuri 10'

Tazama picha hapa:-

Hiyo ni mojawapo ya mbinu mojawapo ambazo wanasiasa wamebuni ya kuwaleta karibu na mwanachi wa kawaida karibu nao.

Wanasiasa wengine wameoneka wakipata chakula na wapiga kura kwenye vibanda, wengine wakiwasaidia wapiga kura katika kazi zao za kila siku na wengine wakishiriki katika kazi mbalimbali za jamii.