Maandalizi ya Ibada ya Kitaifa ya Mazishi ya Rais mstaafu hayati Mwai Kibaki yanaendelea katika uwanja wa Nyayo.
Ibada hiyo itaandaliwa Ijumaa siku moja kabla ya Rais huyo mstaafu kuzikwa Jumamosi nyumbani kwake Othaya, kaunti ya Nyeri.
Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i amewaagiza wananchi kuwa wamewasili kaba ya saa mbili asubuhi, kabla ya mwili huo kuwasili.
Rais mstaafu aliaga dunia siku ya Ijumaa wiki jana, huku habari za kifo chake zikitangazwa na rais Uhuru Kenyatta.
Hizi hapa baadhi ya picha za maandilizi hayo;