Msafara wa mazishi ya hayati Mwai Kibaki umewasili katika uwanja wa Nyayo mwendo wa saa nne unusu asubuhi.
Jeneza linalosheheni mwili wa hayati lilikuwa limefungwa kwa bendera ya Kenya.Kikosi cha wanajeshi wa KDF kilikuwa kimezidikisha jeneza hilo.
Rais Uhuru Kenyatta aliwasili katika uwanja wa Nyayo dakika chache kabla ya ibada ya mazishi ya Mwai Kibaki kung'oa nanga.
Rais alipokelewa na naibu wake William Ruto.
Zaidi ya viongozi 10 wa mataifa mbalimbali ni miongoni mwa wageni maalum ambao wamehudhuria hafla hiyo.