Baadhi ya wabunge la kitaifa wamemtembelea mkewe naibu Rais Dorcas Gachagua kumfariji baada ya kumpoteza dada yake Nancy Muthoni Maina.
Kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook mkewe Naibu Rais alitangaza habari hizo na kuwashukuru viongozi wote waliomtembelea wakati huu wanapitia magumu kama familia.
"Niliguswa na upendo wa wanachama wa Bunge la Kitaifa na Seneti waliokuja kutufariji kufuatia kufiwa na dada yangu, Nancy Muthoni Maina."
Pia alifichua kwamba mbunge wa eneo bunge la Tetu mheshimiwa Geoffrey Wandeto alishiriki kutoka katika kitabu cha Ayubu 2:11-13 kuhusu kuwepo kwa watu wakati wa shida na dhiki, kama marafiki watatu wa Ayubu katika Biblia.
"Mhe. Geoffery Wandeto alishiriki kutoka katika kitabu cha Ayubu 2:11–13 juu ya kuwapo kwa ajili ya watu wakati wa shida na taabu, kama tu marafiki watatu wa Ayubu. Kwa kaka yangu Maina na familia yake, Nakuombea faraja na amani isiyo na mipaka, na mikono yenye huruma ya Mwenyezi Mungu ikushike na kukutia nguvu milele.."