Maandalizi ya mwisho yanaendelea katika uwanja wa Moi, kaunti ya Embu kabla ya sherehe za Madaraka Day.
Kenya inatazamiwa kusherehekea siku yake ya 60 ya Madaraka ambapo wananchi wa tabaka mbalimbali wanatazamiwa kujumuika katika uwanja huo.
Alhamisi asubuhi, wanajeshi walikuwa wakifanya maandalizi ya mwisho huku Wakenya wakiendelea kumiminika katika uwanja huo kuanzia saa mbili asubuhi. Walionekana wakiangalia usalama huku wengine wakitayarisha jukwaa la rais.
Rais William Ruto ndiye ataongoza hafla hiyo.
Zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za Siku ya Madaraka huko Embu.
Siku ya Madaraka ni sikukuu ya kitaifa ambayo husherehekewa kila tarehe 1 Juni kila mwaka ili kuadhimisha kujitawala.