Mkasa wa ajali ya ndege ya kijeshi iliyotokea Alhamisi katika eneo la Elgeyo Marakwet umeacha huzuni kubwa kwa jamii ya wanajeshi, na kuacha familia na marafiki wakiomboleza.
Ndani ya ndege hiyo walikuwepo maafisa waliojitolea maisha yao kwa huduma, ujasiri na wajibu.
Walikuwa ni wapenzi wa mtu, wazazi, watoto au rafiki; kila mmoja na hadithi yake ya kipekee na ndoto.
Katika kuheshimu maisha na taaluma ya kijeshi ya mashujaa hawa walioaga dunia, Rais William Ruto alitangaza kipindi cha siku tatu cha maombolezo kuanzia Ijumaa, Aprili 19, 2024.
Katika kipindi hichi, bendera ya Kenya, ile ya KDF na EAC itapepea nusu mlingoti nchini na misheni za Kenya nje ya nchi.
Hizi hapa nyuso za wanajeshi walioaga;