Kongamano halisi la kwanza kabisa la Wanaume kutokea nchini Kenya lilifanyika katika Carnivore Simba Saloon siku ya Jumanne alasiri.
Hafla hiyo iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Kongamano la Wanaume wa Kujitangaza Stephen Letoo ilianza saa nane mchana na kuendelea hadi baadaye jioni.
Wanaume wa rika tofauti kutoka sehemu mbalimbali za nchi walihudhuria hafla hiyo iliyopambwa na watu kadhaa mashuhuri nchini.
Mfawidhi wa tukio hilo lenye utata alikuwa mchekeshaji Dr Ofweneke pamoja na mtangazaji maarufu Shaffie Weru.
Wanajopo wa Toleo la Kenya la Kongamano la Wanaume la 2023 walijumuisha aliyekuwa Jaji wa Tusker Project Fame Ian Mbugua, wakili maarufu Danstan Omari, Mwanasaikolojia Dkt Frank Njenga, Mjumbe wa Kileleshwa Robert Alai, Mhubiri Simon Mbevi na Chris Kirwa.
Wageni wengine ni pamoja na mwanahabari mkongwe Swaleh Mdoe, kiongozi wa Wachache katika Kaunti ya Nairobi Mhe. Anthony Kiragu Karanja miongoni mwa wengine.
Miongoni mwa mada za siku hiyo ni Afya ya Akili ya Wanaume, Ndoa za wake wengi, Mahusiano, Masuala ya Uzazi Wenza, Talaka na Uzazi.
Tazama Picha la Hafla hiyo:-