(+PICHA)Raila,Kalonzo,Mutua na Ngilu wahudhuria mazishi ya mwendazake Kalembe

Muhtasari
  • Kalembe aliaga dunia mnamo Mei 30 2021, katika hospitali ya Nairobi, baada ya kuugua kwa muda mrefu
  • Viongozi na wanasiasa waliwaongoza wananchi kumuomboleza Kalembe kwa jumbe zao

Kinara wa ODM Raila Odinga na wa Wiper Kalonzo Musyoka Wamehudhuria mazishi yake aliyekuwa mbunge wa Kibwezi Kalembe Ndile, eneo la Mnui Nzau kaunti ya Makueni.

Gavana Charity Ngilu na Alfred Mutua pia wanahudhuria mazishi hayo ambapo mamia ya wakazi wamefurika.

Kalembe aliaga dunia mnamo Mei 30 2021, katika hospitali ya Nairobi, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Viongozi na wanasiasa waliwaongoza wananchi kumuomboleza Kalembe kwa jumbe zao.

Viongozi walimuomboleza kama kiongozi aliyewajali wakazi wa Kibwezi na kuwaakilisha ilivyopaswa bungeni.

Hizi hapa baadhi ya picha za hafla hiyo;

Image: Twitter
Image: Twitter