Polisi aenda mafichoni baada ya kumuua mwenzake kwa kumpiga risasi Nanyuki

Mshukiwa huyo ambaye ametambulishwa kama Titus Keen anadaiwa kutoroka na bunduki aina ya AK-47 iliyojaa risasi baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Muhtasari

•Polisi huyo anaripotiwa kumpiga risasi polisi mwenzake aliyetambulishwa kama Leonard Ojwang siku ya Jumatano katika kituo cha polisi cha Doldol.

Crime scene
Crime scene

Polisi wanamsaka afisa mmoja kutoka kituo kimoja cha polisi katika kaunti ya Laikipia anayedaiwa kumpiga risasi mwenzake na kumuua papo hapo.

Polisi huyo anaripotiwa kumpiga risasi polisi mwenzake aliyetambulishwa kama Leonard Ojwang siku ya Jumatano katika kituo cha polisi cha Doldol.

Mshukiwa huyo ambaye ametambulishwa kama Titus Keen anadaiwa kutoroka na bunduki aina ya AK-47 iliyojaa risasi baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Bado haijabainika kilichoibua mzozo kati ya wawili hao uliopelekea maafa hayo huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika.

Tukio la polisi kuua mwenzake kwa kumpiga risasi  sio jambo geni nchini na hili ni tukio moja  tu la hivi karibuni kuripotiwa.