Mwanamke aua mumewe wa miaka 99 kwa upanga kufuatia mzozo wa chakula Murang'a

Muhtasari

•Baada ya wawili hao kugombana kwa kipindi kifupi Wanjiru alielekea jikoni na kuchukua upanga ambao alitumia kumkata mumewe shingoni na kwenye kichwa.

crime scene
crime scene

Polisi upande wa Kandara kaunti ya Murang'a wanazuilia mwanamke mmoja anayedaiwa kuua mumewe kwa kutumia upanga kufuatia mzozo uliotokea asubuhi ya Jumapili.

Margret Wanjiru, 65, alikamatwa baada ya kumshambulia mumewe Ndung'u Mugachia aliyekuwa amebakisha mwaka mmoja tu kutimiza karne nzima duniani .

Kulingana na DCI, Wanjiru alitumia upanga mkali kumkata mumewe mara mbili; kwenye shingo na kichwani karibu na sikio la kulia

Inaripotiwa kuwa Ndung'u alikuwa ametulia kando ya moto ndani ya nyumba ya mwanawe punde baada ya kuamka wakati mkewe alimpata pale na kuaza malumbano kuhusiana na chakula.

Baada ya wawili hao kugombana kwa kipindi kifupi Wanjiru alielekea jikoni na kuchukua upanga ambao alitumia kumkata mumewe shingoni na kwenye kichwa.

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo amekuwa akimnyanyasa mumewe kwa kumnyima mumewe kwa muda kwa kumnyima chakula.

Wapelelezi wa jinai walifika kwenye eneo la tukio baada ya kupokea ripoti. Mwili wa marehemu ulipelekwa katika mochari ya Gaichanjiru huku upasuaji wa mwili ukisubiriwa.